Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 19:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Na majeslii yaliyo mbinguni yakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa katani safi, nyeupe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Majeshi ya mbinguni yalimfuata yakiwa yamepanda farasi weupe na yamevaa mavazi ya kitani, meupe na safi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Majeshi ya mbinguni yalimfuata yakiwa yamepanda farasi weupe na yamevaa mavazi ya kitani, meupe na safi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Majeshi ya mbinguni yalimfuata yakiwa yamepanda farasi weupe na yamevaa mavazi ya kitani, meupe na safi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Majeshi ya mbinguni walikuwa wakimfuata, wakiwa wamepanda farasi weupe, hali wamevaa mavazi ya kitani safi, nyeupe na nzuri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Majeshi ya mbinguni walikuwa wakimfuata, wakiwa wamepanda farasi weupe, hali wamevaa mavazi ya kitani safi, nyeupe na nzuri.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 19:14
18 Marejeleo ya Msalaba  

Mwambieni binti Sayuni, Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, amepanda punda, Na mwana punda, mtoto wa punda.


Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu sasa hivi, akaniletea zaidi ya majeshi thenashara ya malaika?


Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama thuluji.


na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake,


Na Enok, wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hawo, akisema, Angalia, Bwana alikuja na elfu kumi za watakatifu wake,


NIKAONA, na tazama, Mwana kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arubaini na nne elfu pamoja nae, wenye jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.


Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka khatamu za farasi, mwendo wa mastadio elfu na sita mia.


Hawa watafanya vita na Mwana kondoo, na Mwana kondoo atawashinda, kwa maana ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; nao walioitwa wateule, waaminifu, watashinda pamoja nae.


Nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama farasi mweupe, nae aliyempanda, aitwae Mwaminifu na wa kweli, nae kwa haki ahukumu na kufanya vita.


Nae alipewa kuvikwa kwa katani safi, ya fakhari, kwa maana katani hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.


Lakini unayo majina machache, hatta katika Sardi, watu wasioyatia uchafu mavazi yao. Nao watakwenda pamoja nami katika mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.


Na viti ishirini na vine vilikizuniguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wane, wamekeli, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.


Baada ya haya nikaona, na tazama mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezae kuuhesabu, watu wa killa taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kiti kile cha enzi, na mbele za Mwana Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo