Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 18:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa, wala sauti ya bwana arusi na bibi arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana wafanyi biashara wako walikuwa wakuu wa inchi, kwa kuwa mataifa yote wamedanganywa kwa uchawi wako.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Mwanga wa taa hautaonekana tena ndani yako; sauti za bwana arusi na bibi arusi hazitasikika tena ndani yako. Wafanyabiashara wako walikuwa wakuu duniani, na kwa uchawi wako mataifa yote yalipotoshwa!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Mwanga wa taa hautaonekana tena ndani yako; sauti za bwana arusi na bibi arusi hazitasikika tena ndani yako. Wafanyabiashara wako walikuwa wakuu duniani, na kwa uchawi wako mataifa yote yalipotoshwa!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Mwanga wa taa hautaonekana tena ndani yako; sauti za bwana arusi na bibi arusi hazitasikika tena ndani yako. Wafanyabiashara wako walikuwa wakuu duniani, na kwa uchawi wako mataifa yote yalipotoshwa!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Mwanga wa taa hautaangaza ndani yako tena. Sauti ya bwana arusi na bibi arusi kamwe haitasikika ndani yako tena. Wafanyabiashara wako walikuwa watu maarufu wa dunia. Mataifa yote yalipotoshwa kwa uchawi wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Mwanga wa taa hautaangaza ndani yako tena. Sauti ya bwana arusi na bibi arusi kamwe haitasikika ndani yako tena. Wafanyabiashara wako walikuwa watu maarufu wa dunia. Mataifa yote yalipotoshwa kwa uchawi wako.

Tazama sura Nakili

Ufunuo 18:23
26 Marejeleo ya Msalaba  

Wakamwangalia, kwa maana muda mwingi amewashangaza kwa uchawi wake.

Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.

ambae wafaime wa inchi walizini nae, nao wakaao katika inchi wakalevywa kwa mvinyo ya uasharati wake.

Na katiksi kipaji cha uso wake alikuwa na jina, limeandikwa, SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAILABA NA MACHUKIZO YA INCHI.

Wala sauti ya wapiga vinanda na ya wapiga mazumari na ya wapiga filimbi na ya wapiga baragumu haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala fundi aliye yote wa kazi iliyo yote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa;

kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasharati wake, na wafalme wa inchi wamezini nae, na matajiri ya inchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.

Na wafalme wa inchii waliozini nae na kufanya anasa pamoja nae, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuumgua kwake,

Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.

Bali nje wako mbwa na wachawi na wazinzi na wauaji nao waabuduo sanamu, na killa mtu apendae uwongo na kuufanya.

Wala hapatakuwa usiku huko; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu awatia nuru, nao watamiliki milele hatta milele.

Na wafalme wa dunia, na wakuu, na matajiri, na majemadari, na wenye nguvu, na killa mtumwa, na mungwana, wakajificha katika pango za chini ya miamba ya milima,

Wala hawakutubia mauaji yao, wala uchawi wao, wala uasharati wao, wala kuiba kwao.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo