Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 18:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Akalia kwa nguvu, kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu, umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya killa roho mchafu, na ngome ya killa ndege mchafu mwenye kuchukiza;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Basi, akapaza sauti kwa nguvu akisema, “Umeanguka; Babuloni mkuu umeanguka! Sasa umekuwa makao ya mashetani na pepo wachafu; umekuwa makao ya ndege wachafu na wa kuchukiza mno.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Basi, akapaza sauti kwa nguvu akisema, “Umeanguka; Babuloni mkuu umeanguka! Sasa umekuwa makao ya mashetani na pepo wachafu; umekuwa makao ya ndege wachafu na wa kuchukiza mno.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Basi, akapaza sauti kwa nguvu akisema, “Umeanguka; Babuloni mkuu umeanguka! Sasa umekuwa makao ya mashetani na pepo wachafu; umekuwa makao ya ndege wachafu na wa kuchukiza mno.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Naye akapaza sauti kwa nguvu, akisema: “ ‘Umeanguka! Umeanguka Babeli Mkuu!’ Umekuwa makao ya mashetani na makazi ya kila pepo mchafu, makazi ya kila ndege na kila mnyama achukizaye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Naye akalia kwa nguvu kwa sauti kubwa, akisema: “Umeanguka! Umeanguka Babeli Mkuu! Umekuwa makao ya mashetani na makazi ya kila pepo mchafu, makazi ya kila ndege na kila mnyama achukizaye.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 18:2
26 Marejeleo ya Msalaba  

na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.


Akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia ugurumo saba zikatoa sauti zao.


Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wetu aliposulibiwa.


Malaika mwingine akatoka katika hekalu, kwa santi kuu akimlilia yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvima imekuja; kwa kuwa mavimo ya inchi yamekomaa.


Malaika mwingine akamfuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya hasira ya uasharati wake.


Nikaona roho tatu za uchafu kama vyura zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule nyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uwongo.


Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ilianguka: na Babeli ule mkuu nkakumbukwa mbele za Mungu, ampe kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.


Na yule mwanamke uliyemwona, ndiye mji ule mkubwa, mwenye ufalme juu ya wafalme wa inchi.


Na katiksi kipaji cha uso wake alikuwa na jina, limeandikwa, SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAILABA NA MACHUKIZO YA INCHI.


wakisimama mbali kwa khofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole wake mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio hodari kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.


Na malaika mmoja hodari akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Hivi kwa nguvu nyingi utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana kabisa.


Nikaona malaika mwenye nguvu akikhubiri kwa santi kuu, Nani astahiliye kukifungua kitabu na kuzivunja muhuri zake?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo