Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 18:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitoka machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole wake mji ule ulio mkuu, ambao ndani yake wote wenye merikebu katika bahari walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Wakajimwagia vumbi juu ya vichwa vyao wakilia kwa sauti na kuomboleza: “Ole! Ole kwako mji mkuu! Ni mji ambamo wote wenye meli zisafirizo baharini walitajirika kutokana na utajiri wake. Kwa muda wa saa moja tu umepoteza kila kitu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Wakajimwagia vumbi juu ya vichwa vyao wakilia kwa sauti na kuomboleza: “Ole! Ole kwako mji mkuu! Ni mji ambamo wote wenye meli zisafirizo baharini walitajirika kutokana na utajiri wake. Kwa muda wa saa moja tu umepoteza kila kitu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Wakajimwagia vumbi juu ya vichwa vyao wakilia kwa sauti na kuomboleza: “Ole! Ole kwako mji mkuu! Ni mji ambamo wote wenye meli zisafirizo baharini walitajirika kutokana na utajiri wake. Kwa muda wa saa moja tu umepoteza kila kitu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Nao watajirushia mavumbi vichwani mwao, huku wakilia na kuomboleza, wakisema: “ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa, mji ambao wote wenye meli baharini walitajirika kupitia kwa mali yake! Katika saa moja tu ameangamizwa!’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Nao watajirushia mavumbi vichwani mwao, huku wakilia na kuomboleza, wakisema: “ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa, mji ambao wote wenye meli baharini walitajirika kupitia kwa mali zake! Katika saa moja tu ameangamizwa!

Tazama sura Nakili

Ufunuo 18:19
13 Marejeleo ya Msalaba  

Na zile pembe kumi ulizoziona juu ya nyama, hao watamchukia yule kahaba, na watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kahisa kwa moto.

wakisimama mbali kwa khofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole wake mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio hodari kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.

kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasharati wake, na wafalme wa inchi wamezini nae, na matajiri ya inchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.

Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, manti, na huzuni, na njaa, nae atateketezwa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni hodari.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo