Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 18:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 wakisimama mbali kwa khofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole wake mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio hodari kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Wanasimama kwa mbali kwa sababu ya kuogopa mateso yake na kusema, “Ole! Ole kwako Babuloni, mji maarufu na wenye nguvu! Kwa muda wa saa moja tu adhabu yako imekupata.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Wanasimama kwa mbali kwa sababu ya kuogopa mateso yake na kusema, “Ole! Ole kwako Babuloni, mji maarufu na wenye nguvu! Kwa muda wa saa moja tu adhabu yako imekupata.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Wanasimama kwa mbali kwa sababu ya kuogopa mateso yake na kusema, “Ole! Ole kwako Babuloni, mji maarufu na wenye nguvu! Kwa muda wa saa moja tu adhabu yako imekupata.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Kwa hofu kubwa ya mateso yake, watasimama mbali na kulia na wakisema: “ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa, ee Babeli mji wenye nguvu! Hukumu yako imekuja katika saa moja!’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Kwa hofu kubwa ya mateso yake, watasimama mbali na kulia na wakisema: “ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa, ee Babeli mji wenye nguvu! Hukumu yako imekuja katika saa moja!’

Tazama sura Nakili

Ufunuo 18:10
17 Marejeleo ya Msalaba  

Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wetu aliposulibiwa.

Malaika mwingine akamfuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya hasira ya uasharati wake.

Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ilianguka: na Babeli ule mkuu nkakumbukwa mbele za Mungu, ampe kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.

Na zile pemlbe kumi ulizoziona ni wafalme, ambao hawajaupokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme kwa saa moja pamoja na yule nyama.

wakalia sana, walipouona moshi wa kuungua kwake, wakisema, Ni mji upi ulio mfano wa mji huu mkubwa!

Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitoka machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole wake mji ule ulio mkuu, ambao ndani yake wote wenye merikebu katika bahari walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.

Na malaika mmoja hodari akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Hivi kwa nguvu nyingi utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana kabisa.

Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, manti, na huzuni, na njaa, nae atateketezwa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni hodari.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo