Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 17:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Yule nyama uliyemwona alikuwako, nae hayuko, nae yu tayari kupanda katika abuso na kwenda kwenye uharibifu. Nao wakaao juu ya inchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watataajabu wamwonapo yule nyama, ya kwamba alikuwako, nae hayuko, nae atakuwako.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Huyo mnyama uliyemwona, alikuwa hai hapo awali lakini sasa amekufa. Hata hivyo, karibu sana atapanda kutoka shimoni kuzimu, lakini ataangamizwa. Wanaoishi duniani watashangaa; naam, watu wote ambao majina yao hayakupata kuandikwa katika kitabu cha uhai tangu mwanzo wa ulimwengu, watashangaa kumwona huyo mnyama ambaye hapo awali aliishi, kisha akafa na sasa anatokea tena!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Neno: Bibilia Takatifu

8 Huyo mnyama ambaye ulimwona awali alikuwako, lakini sasa hayuko, naye atapanda kutoka lile Shimo na kwenda kwenye maangamizi yake. Watu wanaoishi duniani ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu kuumbwa kwa ulimwengu watastaajabu kumwona huyo mnyama, kwa maana alikuwako hapo awali, na sasa hayuko, lakini atakuwako baadaye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Huyo mnyama ambaye ulimwona, wakati fulani alikuwepo, lakini sasa hayupo, naye atapanda kutoka lile Shimo na kwenda kwenye maangamizo yake. Watu waishio duniani ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu kuumbwa kwa ulimwengu watastaajabu kumwona huyo mnyama, kwa maana alikuwepo wakati fulani, na sasa hayupo, lakini atakuwepo.

Tazama sura Nakili

Ufunuo 17:8
28 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu:

Lakini msifurahi kwa sababu hii ya kuwa pepo wanawatiini: hali furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni.

Akamsihi asiwaamuru waende zao hatta abusso.

Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Kazi zake zote zimejulika na Mungu tangu mwanzo wa ulimwengu.

kama alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, tuwe watakatifu, wasio khatiya mbele zake, katika pendo.

katika tumaini la nzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema nwongo aliuahidi kabla ya nyakati za zamani;

aliyejuliwa tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifimuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu,

Hatta watakapoumaliza ushuhuda wao yule nyama atokae katika abuso atafanya vifa nao, nae atawashinda na kuwaua.

Na yule nyama aliyekuwako nae hayuko, yeye ndiye wa nane, nae ni mmoja wa wale saba, nae aenenda kwenye uharibifu.

ambae wafaime wa inchi walizini nae, nao wakaao katika inchi wakalevywa kwa mvinyo ya uasharati wake.

Na yule Msingiziaji, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule nyama na yule nabii wa nwongo. Na wataumwa mchana na usiku hatta milele na milele.

Nikawaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele za Mungu; vitabu vikafunuliwa. Kitabu kingine kikafunuliwa, kilicho eha uzima, wafu wakahukumiwa kwa mambo ya matendo yao.

Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

Kwa kuwa ulilishika neno la uvumilivu wangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya inchi.

Yeye ashindae atavikwa mavazi meupe, wala sitalifuta jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitaliungama jina lake mbele za Baba yaugu, na mbele ya malaika zake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo