Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 17:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Nikamwona huyo mwanamke amelewa damu ya watu wa Mungu, na damu ya watu waliouawa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu. Nilipomwona nilishangaa mno.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Nikamwona huyo mwanamke amelewa damu ya watu wa Mungu, na damu ya watu waliouawa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu. Nilipomwona nilishangaa mno.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Nikamwona huyo mwanamke amelewa damu ya watu wa Mungu, na damu ya watu waliouawa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu. Nilipomwona nilishangaa mno.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa kwa damu ya watakatifu, yaani damu ya wale watu waliouawa kwa ushuhuda wa Isa. Nilipomwona huyo mwanamke, nilistaajabu sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa kwa damu ya watakatifu, yaani, damu ya wale watu waliouawa kwa ushuhuda wa Isa. Nilipomwona huyo mwanamke, nilistaajabu sana.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 17:6
12 Marejeleo ya Msalaba  

akamwambia, Killa mtu kwanza huandaa divai iliyo njema, hatta watu wakiisha kunywa sana, ndipo huleta iliyo dhaifu: wewe umeweka divai iliyo njema hatta sasa.


Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali auawe, nikizitunza nguo zao waliomwua.


Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; wala hawakupenda maisha yao hatta wakati wa kufa.


Akapewa kutia pumzi katika sanamu ya nyama, hatta ile sanamu ya nyama inene, na kufanya wo wote wasioisujudu sanamu ya nyama wanawe.


Akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya killa kabila na lugba na taifa.


kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na manabii, nawe umewapa damu, wainywe; nao wamestahili.


Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo