Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 17:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Na katiksi kipaji cha uso wake alikuwa na jina, limeandikwa, SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAILABA NA MACHUKIZO YA INCHI.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Alikuwa ameandikwa juu ya paji la uso wake jina la fumbo “Babuloni mkuu, mama wa wazinzi na wa mambo yote ya kuchukiza sana duniani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Alikuwa ameandikwa juu ya paji la uso wake jina la fumbo “Babuloni mkuu, mama wa wazinzi na wa mambo yote ya kuchukiza sana duniani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Alikuwa ameandikwa juu ya paji la uso wake jina la fumbo “Babuloni mkuu, mama wa wazinzi na wa mambo yote ya kuchukiza sana duniani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kwenye paji lake la uso palikuwa pameandikwa jina la siri: Babeli Mkuu, Mama wa makahaba na wa machukizo ya dunia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kwenye kipaji chake cha uso palikuwa pameandikwa jina: “siri, babeli mkuu, mama wa makahaba na wa machukizo ya dunia.”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 17:5
18 Marejeleo ya Msalaba  

mwisho wao uharibifu, mungu wao tumbo, utukufu wao u katika aibu yao, waniao mambo ya duniani.


lakini yuko azuiae sasa, hatta atakapoondolewa.


Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhababu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, na vile vinara saba ulivyoviona ni makanisa saba.


Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wetu aliposulibiwa.


Malaika mwingine akamfuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya hasira ya uasharati wake.


Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ilianguka: na Babeli ule mkuu nkakumbukwa mbele za Mungu, ampe kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.


AKAJA mmoja wa malaika wale saba wenye vile vichupa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi,


ambae wafaime wa inchi walizini nae, nao wakaao katika inchi wakalevywa kwa mvinyo ya uasharati wake.


Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya nyama amehukuae, mwenye vile vichwa saba na zile pemhe kumi.


Akalia kwa nguvu, kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu, umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya killa roho mchafu, na ngome ya killa ndege mchafu mwenye kuchukiza;


Na malaika mmoja hodari akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Hivi kwa nguvu nyingi utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana kabisa.


kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki: maana amemhukumu yule kahabu mkuu aliyeiharibu inchi kwa uasharati wake, na kumpatiliza kwa ajili va damu ya watumwa wake mkononi mwake.


akisema, Msiidhuru inchi wala bahari wala miti hatta tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mwenyiezi Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo