Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 17:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Maana Muugu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule nyama ufalme hatta maneno ya Mungu yatimizwe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Maana Mungu ametia mioyoni mwao nia ya kutekeleza shabaha yake, yaani wakubaliane wao kwa wao na kumpa huyo mnyama mamlaka yao ya kutawala, mpaka hapo yale aliyosema Mungu yatakapotimia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Maana Mungu ametia mioyoni mwao nia ya kutekeleza shabaha yake, yaani wakubaliane wao kwa wao na kumpa huyo mnyama mamlaka yao ya kutawala, mpaka hapo yale aliyosema Mungu yatakapotimia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Maana Mungu ametia mioyoni mwao nia ya kutekeleza shabaha yake, yaani wakubaliane wao kwa wao na kumpa huyo mnyama mamlaka yao ya kutawala, mpaka hapo yale aliyosema Mungu yatakapotimia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kwa maana Mungu ameweka mioyoni mwao kutimiza kusudi lake kwa kukubali kumpa yule mnyama mamlaka yao ya utawala hadi maneno ya Mungu yatakapotimia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kwa maana Mungu ameweka mioyoni mwao kutimiza kusudi lake kwa kukubali kumpa yule mnyama mamlaka yao ya utawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 17:17
28 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu aenda zake kama ilivyoamriwa; lakini ole wake mtu yule ambae anasalitiwa nae!


Shetani akamwingia Yuda, aitwae Iskariote, nae alikuwa katika hesabu ya wale thenashara.


Kwa maana nawaambieni, Hili lililoandikwa halina buddi kutimizwa kwangu, Alihesabiwa pamoja na maasi; kwa maana linipasalo lina mwisho.


Ikiwa aliwaita wale miungu waliojiliwa na neno la Mungu (na maandiko hayawezi kutanguka),


Sisemi khabari za ninyi nyote: nawajua niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aulae mkate pamoja nami ameinua kisigino chake juu yangu.


Hatta wakati wa chakula cha jioni, Shetani alipokwisha kumtia Yuda, mwana wa Simon Iskariote, moyo wa kumsaliti,


Bassi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani; andiko litimie linenalo, Waligawanya nguo zangu, na vazi langu walilipigia kura. Bassi ndivyo walivyofanya askari.


Baada ya haya Yesu, akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizwa, andiko litimizwe, akasema, Nina kiu.


Lakini Mungu ashukuriwe atiae bidii ile ile kwa ajili yenu katika moyo wa Tito.


isipokuwa katika siku zile za malaika wa saba, atakapokuwa tayari kupiga: hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowakhubiri watumishi wake manabii.


NIKAONA ishara nyingine katika mbingu, kubwa, ya ajabu, malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo hasira ya Mungu imetimia.


Hawa wana shauri amoj, nao wampa yule nyama nguvu zao na mamlaka yao.


Akaniambia, Andika, Wa kheri walioitwa kwa karamu ya arusi ya Mwana Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.


Wakapewa killa mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hatta itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao watakaouawa vile vile kama wao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo