Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 16:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao, wala hawakuyatubia matendo yao.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 wakamtukana Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu yao na madonda yao. Lakini hawakutubu matendo yao mabaya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 wakamtukana Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu yao na madonda yao. Lakini hawakutubu matendo yao mabaya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 wakamtukana Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu yao na madonda yao. Lakini hawakutubu matendo yao mabaya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 wakamlaani Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu na majeraha yao, wala hawakutubu kwa ajili ya matendo yao maovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 wakamlaani Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu na majeraha yao, wala hawakutubu kwa ajili ya matendo yao maovu.

Tazama sura Nakili

Ufunuo 16:11
20 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na wakidanganyika.

Na katika saa ile palikuwa na tetemeko la inchi, nalo kubwa, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka, wana Adamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na khofu wakamtukuza Mungu wa mbingu.

Akaenda wa kwanza, akakimimina kichupa chake juu ya inchi, pakawa jipu baya, ovu, juu ya wale watu wenye alama ya nyama, na wale wenye kuisujudu sanamu yake.

Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kuloka mbinguni juu ya wana Adamu. Wana Adamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe. Maana pigo lake kubwa mno.

Wana Adamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo yote, wala hawtikutubu na kumpa utukufu.

Nami nimempa muda illi atubu uzinzi wake, nae bataki kutubu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo