Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 16:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Malaika wa tano akakimimina kichupa chake juu ya kiti cha enzi cha yule nyama, ufalme wake ukatiwa giza, wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu yao,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Kisha, malaika wa tano akamwaga bakuli lake juu ya makao makuu ya yule mnyama. Giza likauvamia utawala wake, watu wakauma ndimi zao kwa sababu ya maumivu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Kisha, malaika wa tano akamwaga bakuli lake juu ya makao makuu ya yule mnyama. Giza likauvamia utawala wake, watu wakauma ndimi zao kwa sababu ya maumivu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Kisha, malaika wa tano akamwaga bakuli lake juu ya makao makuu ya yule mnyama. Giza likauvamia utawala wake, watu wakauma ndimi zao kwa sababu ya maumivu,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Malaika wa tano akamimina bakuli lake kwenye kiti cha utawala cha yule mnyama, nao ufalme wake ukagubikwa na giza. Watu wakatafuna ndimi zao kwa ajili ya maumivu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Malaika wa tano akamimina bakuli lake kwenye kiti cha enzi cha yule mnyama, nao ufalme wake ukagubikwa na giza. Watu wakatafuna ndimi zao kwa ajili ya maumivu,

Tazama sura Nakili




Ufunuo 16:10
22 Marejeleo ya Msalaba  

na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.


na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.


Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni miguu na mikono, mchukueni mkamtupe katika giza la nje: ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.


atamkata vipande viwili, ataweka sehemu yake pamoja na wanafiki: ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.


bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.


Hapo kutakuwako kulia na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaak na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, na ninyi wenyewe nikitupwa nje.


Heshimuni walu wote. Upendeni udugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.


Nao wakaao juu ya inchi watafanya furaha juu yao ua kushangilia. Na watapelekeana zawadi kwa kuwa manabii hawo wawili waliwatesa wao wakaao juu ya inchi.


Na behewa iliyo nje ya hekalu uitupe nje wala usiipime, kwa maana mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arubaini na miwili.


Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wetu aliposulibiwa.


Maana Muugu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule nyama ufalme hatta maneno ya Mungu yatimizwe.


Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke yule.


Akalia kwa nguvu, kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu, umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya killa roho mchafu, na ngome ya killa ndege mchafu mwenye kuchukiza;


Na malaika mmoja hodari akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Hivi kwa nguvu nyingi utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana kabisa.


wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa, wala sauti ya bwana arusi na bibi arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana wafanyi biashara wako walikuwa wakuu wa inchi, kwa kuwa mataifa yote wamedanganywa kwa uchawi wako.


Malaika wa nne akapiga baragumu, thuluth ya jua ikapigwa, na thuluth ya mwezi, na thuluth ya nyota, illi ile thuluth itiwe giza, mchana usiangaze thuluth yake wala usiku vivyo hivyo.


Akalifungua shimo la abuso; moshi ukapanda kutoka lile shimo kama moshi wa tanuru kubwa: juu na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo