Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 15:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Na mmoja wa wale nyama wane wenye uliayi akawapa vichupa saba vya dhahabu, vimejaa ghadhabu ya Mungu aliye hayi hatta milele na milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Kisha, mmojawapo wa wale viumbe wanne akawapa hao malaika saba mabakuli ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, aishiye milele na milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Kisha, mmojawapo wa wale viumbe wanne akawapa hao malaika saba mabakuli ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, aishiye milele na milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Kisha, mmojawapo wa wale viumbe wanne akawapa hao malaika saba mabakuli ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, aishiye milele na milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Ndipo mmoja wa wale viumbe wanne wenye uhai akawapa wale malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, yeye aishiye milele na milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Ndipo mmoja wa wale viumbe wanne wenye uhai akawapa wale malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, yeye aishiye milele na milele.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 15:7
13 Marejeleo ya Msalaba  

Maana wao wenyewe wanatangaza khabari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu, mkaziacha sanamu illi kumtumikia Mungu aliye hayi, wa kweli,


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


akaapa kwa yeye aliye bayi hatta milele na milele, aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na inchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na muhulla baada ya haya,


yeye nae atakunywa mvinyo ya hasira ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji katika kikombe cha ghadhabu yake, nae ataumwa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika walakalifu na mbele za Mwana kondoo.


NIKAONA ishara nyingine katika mbingu, kubwa, ya ajabu, malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo hasira ya Mungu imetimia.


Akaenda wa kwanza, akakimimina kichupa chake juu ya inchi, pakawa jipu baya, ovu, juu ya wale watu wenye alama ya nyama, na wale wenye kuisujudu sanamu yake.


AKAJA mmoja wa malaika wale saba wenye vile vichupa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi,


Akaja mmoja wa wale malaika saba walio na vichupa vile saba vijaavyo yale mapigo saba ya mwisho, akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi arusi, mke wa Mwana kondoo.


ndipo hawa wazee ishirini na wane watakapoanguka mbele zake aketiye juu ya kiti cha enzi, nao watamsujudu veye aliye hayi hatta milele na milele, nao watatupa taji zao mbele ya kiti eha enzi, wakisema,


Hatta alipokitwaa kile kitabu, nyama wane wenye uhayi na wale wazee ishirini na wane wakaanguka mbele ya Mwana Kondoo, killa mmoja wao ana kinubi, na vitupa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambavyo ni maombi ya watakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo