Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 15:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Nikaona kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, nao wenye kushinda, na kujiepusha na yule nyama na sanamu yake na alama yake, na hesabu ya jina lake, wamesimama juu ya bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Kisha nikaona kitu kama bahari ya kioo, imechanganywa na moto. Nikawaona pia wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake na ambaye jina lake lilitajwa kwa ile tarakimu. Watu hao walikuwa wamesimama kando ya hiyo bahari ya kioo, wakiwa na vinubi walivyopewa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Kisha nikaona kitu kama bahari ya kioo, imechanganywa na moto. Nikawaona pia wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake na ambaye jina lake lilitajwa kwa ile tarakimu. Watu hao walikuwa wamesimama kando ya hiyo bahari ya kioo, wakiwa na vinubi walivyopewa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Nikaona kile kilichoonekana kama bahari ya kioo iliyochanganyikana na moto. Kando ya hiyo bahari, walikuwa wamesimama wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake pamoja na tarakimu ya jina lake. Mikononi mwao walikuwa wameshika vinubi walivyopewa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

Ufunuo 15:2
14 Marejeleo ya Msalaba  

Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

illi kujaribiwa kwake imani yenu, ambako kuna thamani kuu kuliko dbahabu ipoteayo, ijapokuwa imejaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo:

Wapenzi, msione kuwa ni ajahu ule msiba unaowapata kama moto illi mjaribiwe, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho;

Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; wala hawakupenda maisha yao hatta wakati wa kufa.

NIKASIMAMA juu ya mchanga wa bahari. Nikaona nyama akitoka katika bahari niwenye vichwa saba, na pembe kumi, na juu ya pembe zile vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya ukafiri.

Nae awakosesha wakaao juu ya inchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya nyama, akiwaambia wakaao juu ya inchi kumfanyia sanamu yule nyama aliyekuwa na jeraha ya mauti akaishi.

tena kwamba mtu aliye yote asimmne wala kuuza, isipokuwa ana alama ile au jimi la nyama yule, au hesabu ya jina lake.

Na majenzi ya nle ukuta ya yaspi, na mji ule dhahabu safi, mfano wa kioo safi.

Na mliele ya kile kiti cha enzi, mfano wa bahari ya kioo eheupe, kama krustallo, na kati kati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, nyama wane, wamejaa macho mbele na nyuma.

Hatta alipokitwaa kile kitabu, nyama wane wenye uhayi na wale wazee ishirini na wane wakaanguka mbele ya Mwana Kondoo, killa mmoja wao ana kinubi, na vitupa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambavyo ni maombi ya watakatifu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo