Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 15:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NIKAONA ishara nyingine katika mbingu, kubwa, ya ajabu, malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo hasira ya Mungu imetimia.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kisha nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo saba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kisha nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo saba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kisha nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo saba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Ndipo nikaona ishara nyingine kubwa ya ajabu mbinguni: malaika saba wenye yale mapigo saba ya mwisho, kwa sababu kwa mapigo hayo ghadhabu ya Mungu ilikuwa imekamilika.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Ndipo nikaona ishara nyingine kubwa ya ajabu mbinguni: malaika saba wenye yale mapigo saba ya mwisho, kwa sababu kwa mapigo hayo ghadhabu ya Mungu ilikuwa imekamilika.

Tazama sura Nakili

Ufunuo 15:1
21 Marejeleo ya Msalaba  

Akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia ugurumo saba zikatoa sauti zao.

Ole wa pili umekwisha pita, tazama ole wa tatu anakuja upesi.

yeye nae atakunywa mvinyo ya hasira ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji katika kikombe cha ghadhabu yake, nae ataumwa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika walakalifu na mbele za Mwana kondoo.

Malaika yule akautupa mundu wake hatta inchi, akauchuma mzabibu wa inchi, akatupa katika shinikizo la hasira ya Mungu, lile kubwa.

NIKASIKIA sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vichupa vya ghadhabu ya Mungu juu ya inchi.

AKAJA mmoja wa malaika wale saba wenye vile vichupa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi,

Na upanga mkali hutoka kinywani mwake awapige mataifa kwa huo. Nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, nae anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ukali wa ghadhabu ya Mungu Mwenyiezi.

Akaja mmoja wa wale malaika saba walio na vichupa vile saba vijaavyo yale mapigo saba ya mwisho, akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi arusi, mke wa Mwana kondoo.

Nikaona, nikasikia tai akiruka kati kati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya inchi, kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu ya malaika watatu, walio tayari kupiga.

Nikawaona malaika saba wasimamao mbele za Mungu, wakapewa baragumu saba.

Na wale malaika saba wenye baragumu saba wakajifanya tayari illi wazipige.

Na wana Adamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia kazi za mikono yao hatta wasiwasujudu mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za mili, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo