Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 14:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Malaika mwingine akatoka katika hekalu, kwa santi kuu akimlilia yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvima imekuja; kwa kuwa mavimo ya inchi yamekomaa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Kisha malaika mwingine akatoka hekaluni, na kwa sauti kubwa akamwambia yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu, “Tafadhali, tumia mundu wako ukavune mavuno, maana wakati wa mavuno umefika; mavuno ya dunia yameiva.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Kisha malaika mwingine akatoka hekaluni, na kwa sauti kubwa akamwambia yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu, “Tafadhali, tumia mundu wako ukavune mavuno, maana wakati wa mavuno umefika; mavuno ya dunia yameiva.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Kisha malaika mwingine akatoka hekaluni, na kwa sauti kubwa akamwambia yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu, “Tafadhali, tumia mundu wako ukavune mavuno, maana wakati wa mavuno umefika; mavuno ya dunia yameiva.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Kisha malaika mwingine akaja kutoka Hekaluni naye akamwita kwa sauti kubwa yule aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu akasema, “Chukua mundu wako ukavune kwa kuwa wakati wa mavuno umewadia, kwa maana mavuno ya dunia yamekomaa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Kisha malaika mwingine akaja kutoka hekaluni naye akamwita kwa sauti kubwa yule aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu akasema, “Chukua mundu wako ukavune kwa kuwa wakati wa mavuno umewadia, kwa maana mavuno ya dunia yamekomaa.”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 14:15
20 Marejeleo ya Msalaba  

Viacheni vyote vikue hatta wakati wa mavuno: na wakati wa mavuno nitawaambia wavimao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita, mkayachome; bali nganu ikusauyeni ghalani mwangu.


na yule adui aliyeyapanda ni shetani; na mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.


Kajazeni kipimo cha baba zenu.


Hatta matunda yakiiva, marra aupeleka mundu kwa kuwa mavuno yamewadia.


wakituzuia tusiseme na mataifa wapate kuokolewa; illi watimize dhambi zao siku zote; lakini hasira imewafikia hatta mwisho.


Hekalu ya Mungu ikafunguliwa mbinguni na sanduku la agano likaonekana ndani ya hekalu yake. Kukawa umeme, na sauti, na radi, na tetemeko, na mvua ya mawe uyingi sana.


Atumia uweza wote wa nyama yule wa kwanza mbele yake, na kuifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie nyama wa kwanza, ambae jeraha yake ya mauti iliponywa.


Nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa Mwana Adamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono wake mundu mkali.


Na yeye aliyeketi juu ya wingu akautupa mundu wake juu ya inchi, inchi ikavunwa.


Malaika mwingine akatoka katika hekalu iliyo mbinguni, yeye nae ana mundu mkali.


Na malaika mwingine akatoka katika ile madhbabu, mwenye mamlaka juu ya moto; kwa sauti kuu akamlilia yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume matawi va mzabibu wa inchi, maana zabibu zake zimewiva sana.


na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakaloka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, kingʼaacho, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu.


Malaika wa saba akakimimina kichupa chake katika hewa. Sauti kuu ikatoka katika hekalu ya mbinguni, kalika kiti kile cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.


Wakalia kwa sauti kuu, wakiseina, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hatta lini huhukumu na kuipatia haki damu yetu kwao wakaao juu ya inchi?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo