Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 14:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NIKAONA, na tazama, Mwana kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arubaini na nne elfu pamoja nae, wenye jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kisha, nikaona mlima Siyoni na Mwanakondoo amesimama juu yake; pamoja naye walikuwa watu 144,000 ambao juu ya paji za nyuso zao walikuwa wameandikwa jina la Mwanakondoo na jina la Baba yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kisha, nikaona mlima Siyoni na Mwanakondoo amesimama juu yake; pamoja naye walikuwa watu 144,000 ambao juu ya paji za nyuso zao walikuwa wameandikwa jina la Mwanakondoo na jina la Baba yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kisha, nikaona mlima Siyoni na Mwanakondoo amesimama juu yake; pamoja naye walikuwa watu 144,000 ambao juu ya paji za nyuso zao walikuwa wameandikwa jina la Mwanakondoo na jina la Baba yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kisha nikatazama, na hapo mbele yangu Mwana-Kondoo alikuwa amesimama juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa wale elfu mia moja na arobaini na nne wenye jina la Mwana-Kondoo na jina la Baba yake limeandikwa kwenye paji za nyuso zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kisha nikatazama na hapo mbele yangu alikuwepo Mwana-Kondoo, akiwa amesimama juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa wale 144,000 wenye Jina la Mwana-Kondoo na Jina la Baba yake likiwa limeandikwa kwenye vipaji vya nyuso zao.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 14:1
30 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nawaambieni, Killa atakaenikiri mbele za watu, Mwana wa Adamu nae atamkiri mbele za malaika wa Mungu.


kama ilivyoandikwa, Tazama, Naweka katika Sayuni jiwe likwaazalo, na mwamba uangushao: Na killa amwaminiye hataaibishwa.


Nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa Mwana Adamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono wake mundu mkali.


nao waimba wimbo niliouona kuwa mpya mbele ya kili cha enzi, na mbele ya wale nyama wane wenye uhayi, na wale wazee; na hapana mtu aliyeweza kujifunza uimbo ule illa wale mia na arubaini na nne elfu walionunuliwa katika inchi.


Na baada ya haya nikaona, na, tazama, hekalu ya khema ya ushuhuda katika mbingu ilifunguliwa;


Na watumishi wake watamtumikia; nao watamwona uso wake, na jina lake katika vipaji vya nyuso zao.


Yeye ashindae, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, Yerusalemi ulio mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.


BAADA ya haya naliona, na tazama mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hatta huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana buddi kuwa baada ya bayo.


Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Manti, na Kuzimu akafuatana nae. Wakapewa mamlaka juu ya robo ya inchi wane kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa nyama mwitu wa inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo