Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 13:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Wakamsujudu yule joka aliyempa nyama uwezo, wakamsujudu yule nyama, wakisema, Nani afananae na nyama? Nani awezae kufanya vita nae?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Watu wote wakaliabudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake. Wakamwabudu pia huyo mnyama wakisema, “Nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Watu wote wakaliabudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake. Wakamwabudu pia huyo mnyama wakisema, “Nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Watu wote wakaliabudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake. Wakamwabudu pia huyo mnyama wakisema, “Nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Watu wakaliabudu lile joka kwa sababu lilikuwa limempa huyo mnyama mamlaka yake, pia wakamwabudu huyo mnyama na kuuliza, “Ni nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana vita naye?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Watu wakaliabudu lile joka kwa sababu lilikuwa limempa huyo mnyama mamlaka yake, pia wakamwabudu huyo mnyama na kuuliza, “Ni nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana vita naye?”

Tazama sura Nakili

Ufunuo 13:4
18 Marejeleo ya Msalaba  

ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

yule mpingamizi, ajiinuae nafsi yake juu ya killa kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hatta yeye mwenyewe huketi katika hekalu la Mungu, kama Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba ndive Mungu.

Ishara nyingine ikaonekana mbinguni; joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.

Na mkia wake wakokota thuluth ya nyota za mbinguni na kuziangusha katika inchi.

Nikaona nyama mwingine akipanda juu kutoka inchi, nae alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana Kondoo, akanena kama joka.

Akapewa kutia pumzi katika sanamu ya nyama, hatta ile sanamu ya nyama inene, na kufanya wo wote wasioisujudu sanamu ya nyama wanawe.

Na yule nyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubba, na kinywa chake kama kinywa cha simba; yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.

Hawa watafanya vita na Mwana kondoo, na Mwana kondoo atawashinda, kwa maana ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; nao walioitwa wateule, waaminifu, watashinda pamoja nae.

wakalia sana, walipouona moshi wa kuungua kwake, wakisema, Ni mji upi ulio mfano wa mji huu mkubwa!

Na wana Adamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia kazi za mikono yao hatta wasiwasujudu mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za mili, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo