Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 13:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Na yule nyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubba, na kinywa chake kama kinywa cha simba; yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Mnyama huyo niliyemwona alikuwa kama chui; miguu yake kama ya dubu na kinywa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu yake, kiti chake cha enzi na uwezo mkuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Mnyama huyo niliyemwona alikuwa kama chui; miguu yake kama ya dubu na kinywa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu yake, kiti chake cha enzi na uwezo mkuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Mnyama huyo niliyemwona alikuwa kama chui; miguu yake kama ya dubu na kinywa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu yake, kiti chake cha enzi na uwezo mkuu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Mnyama yule niliyemwona alifanana na chui, lakini miguu yake ilikuwa kama ya dubu na kichwa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu zake, kiti chake cha utawala na mamlaka makubwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Mnyama yule niliyemwona alifanana na chui, lakini miguu yake ilikuwa kama ya dubu na kichwa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu zake, kiti chake cha enzi na mamlaka makubwa.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 13:2
27 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, illi kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, mataifa wrote wakasikie; nikaokolewa katika kanwa la simba.


Erevukeni, kesheni; kwa kuwa mshitaki wenu Shetani, kama simba angurumae, huzungukazunguka, akitafuta mtu amle;


Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika inchi alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.


Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyunia ya mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.


Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.


Atumia uweza wote wa nyama yule wa kwanza mbele yake, na kuifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie nyama wa kwanza, ambae jeraha yake ya mauti iliponywa.


Wakamsujudu yule joka aliyempa nyama uwezo, wakamsujudu yule nyama, wakisema, Nani afananae na nyama? Nani awezae kufanya vita nae?


Malaika wa tano akakimimina kichupa chake juu ya kiti cha enzi cha yule nyama, ufalme wake ukatiwa giza, wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu yao,


Na zile pemlbe kumi ulizoziona ni wafalme, ambao hawajaupokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme kwa saa moja pamoja na yule nyama.


Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;


Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.


Akamshika joka, yule nyoka wa zamani, aliye msingiziaji, Shetani, akamfunga miaka elfu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo