Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 13:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Nae awahinya wote, wadogo na wakuu na matajiri na maskini na walio huru na watumwa, watiwe alama katika mkono wao wa kuume au katika vipaji vya nyuso zao:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Aliwalazimisha wote, wadogo na wakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa, watiwe alama juu ya mikono yao ya kulia au juu ya paji za nyuso zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Aliwalazimisha wote, wadogo na wakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa, watiwe alama juu ya mikono yao ya kulia au juu ya paji za nyuso zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Aliwalazimisha wote, wadogo na wakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa, watiwe alama juu ya mikono yao ya kulia au juu ya paji za nyuso zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Pia alimlazimisha kila mmoja, mdogo na mkubwa, tajiri na maskini, mtu huru na mtumwa, atiwe chapa kwenye mkono wake wa kuume au kwenye paji la uso wake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Pia alimlazimisha kila mmoja, mdogo na mkubwa, tajiri na maskini, mtu huru na mtumwa, atiwe chapa kwenye mkono wake wa kuume au kwenye kipaji chake cha uso,

Tazama sura Nakili




Ufunuo 13:16
26 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi nikiisha kuupata msaada utokao kwa Mungu nimesimama hatta leo hivi nikiwashuhudia wadogo kwa wakubwa, wala sisemi neno illa yale ambayo manabii na Musa waliyasema, kwamba yatakuwa;


Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa tukaingia katika mwili mmoja, ikiwa tu Wayahudi, au ikiwa tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.


Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.


Tangu sasa mtu asinitie taabu; kwa maana ninachiukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.


mkijua ya kuwa killa neno jema atendalo mtu, atapewa lilo hilo na Bwana, akiwa ni mtumwa, au akiwa ni huru.


Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mshenzi wala Mskuthi, mtumwa wala mungwana, bali Kristo ni yote, na katika wote.


Vile vile kama Yanne na Yambre walivyopingana na Mnsa, vivyo hivyo na hawa wapingana na kweli, ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.


Na mataifa walighadhabika, ghadhabu yako ikaja, na wakati wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, nao walichao jina lako, wadogo na wakubwa, na wa kuwaharibu hawo waiharibuo inchi.


Nikaona kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, nao wenye kushinda, na kujiepusha na yule nyama na sanamu yake na alama yake, na hesabu ya jina lake, wamesimama juu ya bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.


mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya maakida, na nyama ya watu hodari na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana na watumwa, wadogo na wakubwa.


Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;


Sauti ikatoka katika kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumishi wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo na wakuu.


Nikawaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele za Mungu; vitabu vikafunuliwa. Kitabu kingine kikafunuliwa, kilicho eha uzima, wafu wakahukumiwa kwa mambo ya matendo yao.


Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.


Na wafalme wa dunia, na wakuu, na matajiri, na majemadari, na wenye nguvu, na killa mtumwa, na mungwana, wakajificha katika pango za chini ya miamba ya milima,


akisema, Msiidhuru inchi wala bahari wala miti hatta tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mwenyiezi Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo