Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 13:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Nae awakosesha wakaao juu ya inchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya nyama, akiwaambia wakaao juu ya inchi kumfanyia sanamu yule nyama aliyekuwa na jeraha ya mauti akaishi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Aliwapotosha wakazi wa dunia kwa miujiza hiyo aliyojaliwa kutenda mbele ya mnyama wa kwanza. Aliwaambia wakazi wa dunia watengeneze sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi tena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Aliwapotosha wakazi wa dunia kwa miujiza hiyo aliyojaliwa kutenda mbele ya mnyama wa kwanza. Aliwaambia wakazi wa dunia watengeneze sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi tena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Aliwapotosha wakazi wa dunia kwa miujiza hiyo aliyojaliwa kutenda mbele ya mnyama wa kwanza. Aliwaambia wakazi wa dunia watengeneze sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi tena.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kwa sababu ya zile ishara alizokuwa amepewa uwezo wa kuzifanya kwa niaba ya yule mnyama wa kwanza, akawadanganya watu walioishi duniani. Akawaamuru wasimamishe sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kwa sababu ya zile ishara alizokuwa amepewa uwezo wa kuzifanya kwa niaba ya yule mnyama wa kwanza, akawadanganya wakaao duniani. Akawaamuru wasimamishe sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 13:14
29 Marejeleo ya Msalaba  

yule mpingamizi, ajiinuae nafsi yake juu ya killa kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hatta yeye mwenyewe huketi katika hekalu la Mungu, kama Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba ndive Mungu.


Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.


NIKASIMAMA juu ya mchanga wa bahari. Nikaona nyama akitoka katika bahari niwenye vichwa saba, na pembe kumi, na juu ya pembe zile vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya ukafiri.


Akapewa kutia pumzi katika sanamu ya nyama, hatta ile sanamu ya nyama inene, na kufanya wo wote wasioisujudu sanamu ya nyama wanawe.


Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.


Na moshi wa maumivu yao wapanda juu hatta milele na milele, nao bawana raha mchana na usiku, bao wamsujuduo nyama na sanamu yake, na killa aipokeae alama ya jina lake.


Malaika wa tatu akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu akimsujudu nyama na sanamu yake, na kupokea alama katika kipaji cha uso wake au katika mkono wake,


Nikaona kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, nao wenye kushinda, na kujiepusha na yule nyama na sanamu yake na alama yake, na hesabu ya jina lake, wamesimama juu ya bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.


Nikaona roho tatu za uchafu kama vyura zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule nyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uwongo.


Akaenda wa kwanza, akakimimina kichupa chake juu ya inchi, pakawa jipu baya, ovu, juu ya wale watu wenye alama ya nyama, na wale wenye kuisujudu sanamu yake.


wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa, wala sauti ya bwana arusi na bibi arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana wafanyi biashara wako walikuwa wakuu wa inchi, kwa kuwa mataifa yote wamedanganywa kwa uchawi wako.


Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;


Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Na yule Msingiziaji, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule nyama na yule nabii wa nwongo. Na wataumwa mchana na usiku hatta milele na milele.


Kwa kuwa ulilishika neno la uvumilivu wangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo