Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 13:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Atumia uweza wote wa nyama yule wa kwanza mbele yake, na kuifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie nyama wa kwanza, ambae jeraha yake ya mauti iliponywa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Alikuwa na mamlaka kamili kutoka kwa yule mnyama wa kwanza, na akautumia uwezo huo mbele ya huyo mnyama. Akailazimisha dunia yote na wote waliomo humo kumwabudu huyo mnyama wa kwanza ambaye alikuwa na jeraha la kifo lililokuwa limepona.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Alikuwa na mamlaka kamili kutoka kwa yule mnyama wa kwanza, na akautumia uwezo huo mbele ya huyo mnyama. Akailazimisha dunia yote na wote waliomo humo kumwabudu huyo mnyama wa kwanza ambaye alikuwa na jeraha la kifo lililokuwa limepona.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Alikuwa na mamlaka kamili kutoka kwa yule mnyama wa kwanza, na akautumia uwezo huo mbele ya huyo mnyama. Akailazimisha dunia yote na wote waliomo humo kumwabudu huyo mnyama wa kwanza ambaye alikuwa na jeraha la kifo lililokuwa limepona.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Akatumia mamlaka yote ya yule mnyama wa kwanza kwa niaba yake, naye akaifanya dunia na wote walioishi duniani kumwabudu yule mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Akatumia mamlaka yote ya yule mnyama wa kwanza kwa niaba yake, naye akawafanya wote wakaao duniani kumwabudu yule mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 13:12
12 Marejeleo ya Msalaba  

yule mpingamizi, ajiinuae nafsi yake juu ya killa kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hatta yeye mwenyewe huketi katika hekalu la Mungu, kama Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba ndive Mungu.


Na yule nyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubba, na kinywa chake kama kinywa cha simba; yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.


Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.


Na moshi wa maumivu yao wapanda juu hatta milele na milele, nao bawana raha mchana na usiku, bao wamsujuduo nyama na sanamu yake, na killa aipokeae alama ya jina lake.


Malaika wa tatu akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu akimsujudu nyama na sanamu yake, na kupokea alama katika kipaji cha uso wake au katika mkono wake,


Akaenda wa kwanza, akakimimina kichupa chake juu ya inchi, pakawa jipu baya, ovu, juu ya wale watu wenye alama ya nyama, na wale wenye kuisujudu sanamu yake.


Yule nyama uliyemwona alikuwako, nae hayuko, nae yu tayari kupanda katika abuso na kwenda kwenye uharibifu. Nao wakaao juu ya inchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watataajabu wamwonapo yule nyama, ya kwamba alikuwako, nae hayuko, nae atakuwako.


Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;


Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo