Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 13:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Mtu akichukua mateka achukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hivyo ndivyo uvumilivu na imani ya watakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Aliyepangiwa kuchukuliwa mateka lazima atatekwa; wa kuuawa kwa upanga atauawa kwa upanga. Hivyo, watu wa Mungu na wawe na uvumilivu na imani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Aliyepangiwa kuchukuliwa mateka lazima atatekwa; wa kuuawa kwa upanga atauawa kwa upanga. Hivyo, watu wa Mungu na wawe na uvumilivu na imani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Aliyepangiwa kuchukuliwa mateka lazima atatekwa; wa kuuawa kwa upanga atauawa kwa upanga. Hivyo, watu wa Mungu na wawe na uvumilivu na imani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 “Ikiwa mtu ni wa kuchukuliwa mateka, atachukuliwa mateka. Ikiwa mtu ni wa kuuawa kwa upanga, atauawa kwa upanga.” Hapa ndipo penye wito wa subira na imani ya watakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Ikiwa mtu ni wa kuchukuliwa mateka, atachukuliwa mateka. Ikiwa mtu ni wa kuuawa kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye wito wa subira na imani ya watakatifu.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 13:10
29 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake: maana wote washikao upanga, wataangamia kwa upanga.


Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa: na kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.


Kwa subira yenu mtazipata robo zenu.


mkiwezeshwa kwa nwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya killa namna na uvumilivu pamoja na furaha;


illi msiwe wavivu, hali wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imaui na uvumilivu.


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Na mataifa walighadhabika, ghadhabu yako ikaja, na wakati wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, nao walichao jina lako, wadogo na wakubwa, na wa kuwaharibu hawo waiharibuo inchi.


Hapo ndipo penye uvumilivu wa watakatifu wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.


kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na manabii, nawe umewapa damu, wainywe; nao wamestahili.


Na yule nyama aliyekuwako nae hayuko, yeye ndiye wa nane, nae ni mmoja wa wale saba, nae aenenda kwenye uharibifu.


Yule nyama uliyemwona alikuwako, nae hayuko, nae yu tayari kupanda katika abuso na kwenda kwenye uharibifu. Nao wakaao juu ya inchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watataajabu wamwonapo yule nyama, ya kwamba alikuwako, nae hayuko, nae atakuwako.


Najua matendo yako na upendo wako na khuduma yako na uaminifu wako na uvumilivu wako na matendo yako; tena matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.


Najua matendo yako, na taabu yako, na uvumilivu wako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa wawongo;


Kwa kuwa ulilishika neno la uvumilivu wangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya inchi.


Bassi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Illakini usipokesha nitakuja kwako kama mwizi, nawe hutaijua saa nitakayokuja kwako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo