Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 12:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, illi azaapo, amle mtoto wake. Akazaa mtoto mwanamume, atakaewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hatta kwa Mungu na kwa kiti cbake cha enzi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Kisha, mama huyo akajifungua mtoto wa kiume ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakini mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Kisha, mama huyo akajifungua mtoto wa kiume ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakini mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Kisha, mama huyo akajifungua mtoto wa kiume ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakini mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Yule mwanamke akazaa mtoto wa kiume, atakayeyatawala mataifa yote kwa fimbo ya utawala ya chuma. Lakini huyo mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu kwenye kiti chake cha enzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Yule mwanamke akazaa mtoto mwanaume, atakayeyatawala mataifa yote kwa fimbo yake ya utawala ya chuma. Lakini huyo mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu kwenye kiti chake cha enzi.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 12:5
14 Marejeleo ya Msalaba  

akamchukua mkewe; asimjue kamwe hatta alipomzaa mwanawe wa kifungua mimba; akainwita jina lake YESU.


Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


Namjua mtu mmoja katika Kristo, impita sasa miaka arobatashara, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui, Mungu ajua). Mtu huyu alichukuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.


ya kuwa alichukuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwana Adamu ayanene.


Nikasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hatta huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.


Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika inchi alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.


Nae alikuwa ana mimba, akilia, akiwa ana utungu na kuumwa katika kuzaa.


Na upanga mkali hutoka kinywani mwake awapige mataifa kwa huo. Nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, nae anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ukali wa ghadhabu ya Mungu Mwenyiezi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo