Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 12:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Joka akamkasirikia mwanamke akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Basi, joka hilo likamkasirikia huyo mama, likajiondokea, likaenda kupigana na wazawa wengine wa huyo mama, yaani wote wanaotii amri za Mungu na kumshuhudia Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Basi, joka hilo likamkasirikia huyo mama, likajiondokea, likaenda kupigana na wazawa wengine wa huyo mama, yaani wote wanaotii amri za Mungu na kumshuhudia Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Basi, joka hilo likamkasirikia huyo mama, likajiondokea, likaenda kupigana na wazawa wengine wa huyo mama, yaani wote wanaotii amri za Mungu na kumshuhudia Yesu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke na likaondoka ili kupigana vita na wazawa waliosalia wa huyo mwanamke, yaani wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke na likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Isa Al-Masihi. Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 12:17
26 Marejeleo ya Msalaba  

mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: nti tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin.


Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.


NAMI nilipokuja kwenu ndugu, sikuja niwakhubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.


Erevukeni, kesheni; kwa kuwa mshitaki wenu Shetani, kama simba angurumae, huzungukazunguka, akitafuta mtu amle;


Na hivi twajua ya kuwa tumemjua, ikiwa tunashika amri zake.


Amwaminiye Mwana wa Mungu anao ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini ushuhuda ambao Mungu amemsbuhudia Mwana wake.


Hivi twajua kwamba twawapencla watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.


aliyeshuhudia Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo, mambo yote aliyoyaona.


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Hatta watakapoumaliza ushuhuda wao yule nyama atokae katika abuso atafanya vifa nao, nae atawashinda na kuwaua.


Inchi ikamsaidia mwanamke, inchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.


Akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya killa kabila na lugba na taifa.


Hapo ndipo penye uvumilivu wa watakatifu wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.


Hawa watafanya vita na Mwana kondoo, na Mwana kondoo atawashinda, kwa maana ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; nao walioitwa wateule, waaminifu, watashinda pamoja nae.


Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.


Furahini juu yake, enyi mbingu, na ninyi watakatifu na mitume na manabii, kwa maana Mungu amehukumu hukumu yenu juu yake.


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Nikamwonu nyama, na wafalme wa inchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, na na majeshi yake.


Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.


Wa kheri wazifuazo nguo zao, wawe na amri kuuendea mti wa uzima, na kuuingia mji kwa milango yake.


Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhbahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo