Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 12:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Kwa hiyo shangilieni, mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa inchi na bahari: kwa maana yule msingiziaji ameshuka kwao mwenye hasira nyingi, akijua ya kuwa ana wakati si mwingi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Kwa sababu hiyo, furahini enyi mbingu na vyote vilivyomo ndani yenu. Lakini, ole wenu nchi na bahari, maana Ibilisi amewajieni akiwa na ghadhabu kuu, kwa sababu anajua kwamba muda wake uliobakia ni mfupi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Kwa sababu hiyo, furahini enyi mbingu na vyote vilivyomo ndani yenu. Lakini, ole wenu nchi na bahari, maana Ibilisi amewajieni akiwa na ghadhabu kuu, kwa sababu anajua kwamba muda wake uliobakia ni mfupi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Kwa sababu hiyo, furahini enyi mbingu na vyote vilivyomo ndani yenu. Lakini, ole wenu nchi na bahari, maana Ibilisi amewajieni akiwa na ghadhabu kuu, kwa sababu anajua kwamba muda wake uliobakia ni mfupi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kwa hiyo furahini, ninyi mbingu na wote wanaoishi humo! Lakini ole wenu nchi na bahari, kwa maana huyo ibilisi ameshuka kwenu, akiwa amejaa ghadhabu, kwa sababu anajua ya kuwa muda wake ni mfupi!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kwa hiyo, furahini ninyi mbingu na wote wakaao humo! Lakini ole wenu nchi na bahari, kwa maana huyo ibilisi ameshuka kwenu, akiwa amejaa ghadhabu, kwa sababu anajua ya kuwa muda wake ni mfupi!”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 12:12
18 Marejeleo ya Msalaba  

Kadhalika nawaambia ninyi, iko furaha mbele ya malaika zake Mungu kwa mwenye dhambi mmoja atubuye.


Utukufu una Mungu palipo juu, Na katika inchi amani, kwa watu aliowaridhia.


Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajae atakuja, wala hatakawia.


Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu kama siku moja.


akaapa kwa yeye aliye bayi hatta milele na milele, aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na inchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na muhulla baada ya haya,


Nao wakaao juu ya inchi watafanya furaha juu yao ua kushangilia. Na watapelekeana zawadi kwa kuwa manabii hawo wawili waliwatesa wao wakaao juu ya inchi.


Ole wa pili umekwisha pita, tazama ole wa tatu anakuja upesi.


Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.


Akafunna kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.


Furahini juu yake, enyi mbingu, na ninyi watakatifu na mitume na manabii, kwa maana Mungu amehukumu hukumu yenu juu yake.


Nikaona, nikasikia tai akiruka kati kati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya inchi, kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu ya malaika watatu, walio tayari kupiga.


Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado ziko ole mbili, zinakuja baadae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo