Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 12:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NA ishara kuu ilionekana mbiuguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota thenashara.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kisha, ishara kubwa ikaonekana mbinguni: Mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kisha, ishara kubwa ikaonekana mbinguni: Mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kisha, ishara kubwa ikaonekana mbinguni: mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na taji lenye nyota kumi na mbili lilikuwa kichwani mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ukiwa chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa kichwani mwake.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 12:1
35 Marejeleo ya Msalaba  

Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakinena, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako.


ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni: ndipo mataifa yote ya ulimwengu wataomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbingu kwa nguvu pamoja na utukufu mwingi.


na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika.


kutakuwa na matetemeko makubwa ya inchi mahali mahali, na njaa, na tauni. Kutakuwa na mambo ya kutisha, na ishara kuu kutoka mbinguni.


Na kutakuwa ishara katika jua na mwezi na nyota: na katika inchi dhiiki ya mataifa, wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake;


Aliye nae bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi anaesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi: bassi hii furaha yangu imetimia.


Nitatoa ajabu katika mbingu juu, Na ishara katika inchi chini, Damu na moto, na mvuke wa moshi:


Bali mvaeni Bwana Yesu, wala msitafakari mahitaji ya mwili, nisije mkawasha tamaa zake.


ni haki ya Mungu, ipatwayo kwa kuwa na imani kwa Yesu Kristo, huja kwa watu wote, huwakalia watu wote waaminio.


Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; maana naliwaposea mume mmoja, nimletee Kristo bikira safi.


Maana ninyi nyote mliobatizwa na kuingizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.


Bali Yerusalemi wa juu ni mwungwana, ndio mama yetu sisi.


Lakini mimi, hasha nisijisifie kitu illa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.


Hii ni siri kubwa; lakini nanena khabari ya Kristo na Kanisa.


Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhababu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, na vile vinara saba ulivyoviona ni makanisa saba.


Hekalu ya Mungu ikafunguliwa mbinguni na sanduku la agano likaonekana ndani ya hekalu yake. Kukawa umeme, na sauti, na radi, na tetemeko, na mvua ya mawe uyingi sana.


Ishara nyingine ikaonekana mbinguni; joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.


NIKAONA ishara nyingine katika mbingu, kubwa, ya ajabu, malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo hasira ya Mungu imetimia.


Na ukuta wa mji una misingi thenashara, na katika ile misingi majina theriashara ya mitume wa Mwana kondoo.


Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi uuangaze, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo