Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 11:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wetu aliposulibiwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Maiti zao zitabaki katika barabara za mji mkuu ambapo Bwana wao alisulubiwa. Jina la kupanga la mji huo ni Sodoma au Misri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Maiti zao zitabaki katika barabara za mji mkuu ambapo Bwana wao alisulubiwa. Jina la kupanga la mji huo ni Sodoma au Misri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Maiti zao zitabaki katika barabara za mji mkuu ambapo Bwana wao alisulubiwa. Jina la kupanga la mji huo ni Sodoma au Misri.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa, ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri, ambapo pia Isa Bwana wao alisulubiwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa, ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri, ambapo pia Isa Bwana wao alisulubiwa.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 11:8
40 Marejeleo ya Msalaba  

Amin, nawaambieni, Itakuwa rakhisi inchi ya Sodoma na Gomora istahimili adhabu yao siku ya hukumu, kuliko mji ule.


Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Saul, Saul, mbona wanifukuza?


Kwa ajili hii Yesu nae, illi awatakase watu wake kwa damu yake miwenyewe, alitesyia nje ya mlango.


wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hatta wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu marra ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.


akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipiudua ua kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya;


Kama vile bodoma na Gomora, na miji iliyozunguka, waliofuata uasharati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wamepasiwa hukumu yamoto wa milele.


Na katika saa ile palikuwa na tetemeko la inchi, nalo kubwa, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka, wana Adamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na khofu wakamtukuza Mungu wa mbingu.


Na watu wa hawo jamaa na kabila na lugha na taifa wataitazama mizoga yao siku tatu u nussu, wala hawataiacha mizoga yao kuwekwa kaburini.


Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka khatamu za farasi, mwendo wa mastadio elfu na sita mia.


Malaika mwingine akamfuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya hasira ya uasharati wake.


Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ilianguka: na Babeli ule mkuu nkakumbukwa mbele za Mungu, ampe kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.


AKAJA mmoja wa malaika wale saba wenye vile vichupa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi,


Na yule mwanamke uliyemwona, ndiye mji ule mkubwa, mwenye ufalme juu ya wafalme wa inchi.


Na katiksi kipaji cha uso wake alikuwa na jina, limeandikwa, SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAILABA NA MACHUKIZO YA INCHI.


wakisimama mbali kwa khofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole wake mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio hodari kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.


wakalia sana, walipouona moshi wa kuungua kwake, wakisema, Ni mji upi ulio mfano wa mji huu mkubwa!


Akalia kwa nguvu, kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu, umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya killa roho mchafu, na ngome ya killa ndege mchafu mwenye kuchukiza;


Na malaika mmoja hodari akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Hivi kwa nguvu nyingi utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana kabisa.


Na ndani yake ilionekana damu ya manabii na ya watakatifu na ya wale wote waliouawa juu ya inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo