Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 11:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uitupe nje wala usiipime, kwa maana mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arubaini na miwili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Lakini uache ukumbi ulio nje ya hekalu; usiupime, maana huo umekabidhiwa watu wa mataifa mengine, ambao wataukanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arubaini na miwili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Lakini uache ukumbi ulio nje ya hekalu; usiupime, maana huo umekabidhiwa watu wa mataifa mengine, ambao wataukanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arubaini na miwili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Lakini uache ukumbi ulio nje ya hekalu; usiupime, maana huo umekabidhiwa watu wa mataifa mengine, ambao wataukanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arubaini na miwili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Lakini usiupime ua wa nje wa Hekalu; uache, kwa sababu ua huo wamepewa watu wa Mataifa. Hao wataukanyagakanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na mbili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Lakini usiupime ua wa nje wa Hekalu, uache, kwa sababu ua huo wamepewa watu wa Mataifa. Hao wataukanyagakanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 11:2
32 Marejeleo ya Msalaba  

nao wakiisha kutoka makaburini, baada ya kufufuka kwake, wakaingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.


Kisha Shetani akamchukua hatta mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu, akamwambia,


Ninyi ni chumvi ya dunia: lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwani ikolee? Haifai tena kabisa, illa kufupwa nje na kukanyagwa na watu.


Nao wataanguka kwa ukali wa upanga, watachukuliwa mateka mpaka mataifa yote: nao Yerusalemi utakanyagwa na mataifa, hatta majira ya mataifa yatakapotimia.


Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa nayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho ya neema?


Na baada ya siku tatu u nussu roho ya uhayi itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama, khofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.


Nami nitawarukhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na miateen na sittini, wamevikwa mavazi ya kigunia.


Yule mwanamke akakimbilia nyikani ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, illi wamlishe huku siku elfu na miateen na sittini.


Akanichukua katika Roho hatta mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemi, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyiezi Mungu,


Nami Yohana nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemi mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.


Na mtu aliye yote akiondoa baadhi ya maaeno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika kile kitabu cha uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao khabari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo