Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 11:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Na mataifa walighadhabika, ghadhabu yako ikaja, na wakati wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, nao walichao jina lako, wadogo na wakubwa, na wa kuwaharibu hawo waiharibuo inchi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Watu wa mataifa waliwaka hasira, lakini ghadhabu yako imefika, naam wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii, watakatifu na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wa kuwaangamiza waangamizi wa dunia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Watu wa mataifa waliwaka hasira, lakini ghadhabu yako imefika, naam wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii, watakatifu na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wa kuwaangamiza waangamizi wa dunia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Watu wa mataifa waliwaka hasira, lakini ghadhabu yako imefika, naam wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii, watakatifu na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wa kuwaangamiza waangamizi wa dunia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Mataifa walikasirika; nao wakati wa ghadhabu yako umewadia. Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa, na kuwapa thawabu watumishi wako manabii, na watakatifu wako pamoja na wale wote wanaoliheshimu Jina lako, wakubwa kwa wadogo: na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Mataifa walikasirika nao wakati wa ghadhabu yako umewadia. Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa na kuwapa thawabu watumishi wako manabii na watakatifu wako pamoja na wale wote wanaoliheshimu Jina lako, wakubwa kwa wadogo: na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 11:18
48 Marejeleo ya Msalaba  

Furahini, shangilieni: kwakuwa thawabu yenu nyingi mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.


Na rehema zake vizazi hatta vizazi Kwao wanaomcha.


Na jinsi watu wanavyowekewa kufa marra moja, na baada ya kufa hukumu:


isipokuwa katika siku zile za malaika wa saba, atakapokuwa tayari kupiga: hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowakhubiri watumishi wake manabii.


Na behewa iliyo nje ya hekalu uitupe nje wala usiipime, kwa maana mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arubaini na miwili.


Mtu akichukua mateka achukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hivyo ndivyo uvumilivu na imani ya watakatifu.


Nae awahinya wote, wadogo na wakuu na matajiri na maskini na walio huru na watumwa, watiwe alama katika mkono wao wa kuume au katika vipaji vya nyuso zao:


yeye nae atakunywa mvinyo ya hasira ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji katika kikombe cha ghadhabu yake, nae ataumwa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika walakalifu na mbele za Mwana kondoo.


NIKAONA ishara nyingine katika mbingu, kubwa, ya ajabu, malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo hasira ya Mungu imetimia.


Na mmoja wa wale nyama wane wenye uliayi akawapa vichupa saba vya dhahabu, vimejaa ghadhabu ya Mungu aliye hayi hatta milele na milele.


Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mardufu kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikomhe kile alichokichanganisha, mchanganishieni mardufu.


Na upanga mkali hutoka kinywani mwake awapige mataifa kwa huo. Nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, nae anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ukali wa ghadhabu ya Mungu Mwenyiezi.


mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya maakida, na nyama ya watu hodari na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana na watumwa, wadogo na wakubwa.


Sauti ikatoka katika kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumishi wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo na wakuu.


Nikawaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele za Mungu; vitabu vikafunuliwa. Kitabu kingine kikafunuliwa, kilicho eha uzima, wafu wakahukumiwa kwa mambo ya matendo yao.


Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.


Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami kumlipa killa mtu kama itakavyokuwa kazi yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo