Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 11:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 wakisema, Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyiezi, ulioko, na nliyekuwako, kwa sababu umetwaa uweza wako ulio mkuu, ukamiliki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 wakisema: “Tunakushukuru ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu, uliyeko na uliyekuwako! Maana umetumia nguvu yako kuu, ukaanza kutawala!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 wakisema: “Tunakushukuru ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu, uliyeko na uliyekuwako! Maana umetumia nguvu yako kuu, ukaanza kutawala!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 wakisema: “Tunakushukuru ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu, uliyeko na uliyekuwako! Maana umetumia nguvu yako kuu, ukaanza kutawala!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 wakisema: “Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa kuwa umetwaa uweza wako mkuu na ukaanza kutawala.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 wakisema: “Tunakushukuru, bwana Mwenyezi Mungu, uliyeko na uliyekuwako, kwa kuwa umetwaa uweza wako mkuu na ukaanza kutawala.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 11:17
27 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo:


Saa ileile Yesu akashangilia katika Roho, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na busara mambo haya, ukawafunulia watoto wachanga: Naam, Baba, kwa maana ndivyo vilivyokuwa vinapendeza mbele yako.


Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.


Mungu ashukuriwe, anaetushangiliza daima katika Kristo, na kuyadhihirisha manukato ya hawa wamjuao killa pahali kwa kazi yetu.


Mungu ashukuriwe kwa sababa ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu ipasavyo.


Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu aliyenitia nguvu, kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akiniweka katika khuduma yake;


Yohana kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwake yeye alioko na aliyekuwako nii atakaekuwako: na zitokazo kwa roho saba zilizo mbele ya kiti chake cha enzi:


Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisiio, asema Bwana Mungu, alioko, aliyekuwako, na atakaekuwako, Mwenyiezi.


Malaika wa saha akapiga baragumu, pakawa sauti kuu katika mbingu, zikisema, Falme za dunia zimekwisha kuwa ufalme na Mungu na wa Kristo wake, nae atamiliki hatta milele na milele.


Nao wauimba uimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na uimbo wa Mwana kondoo, wakisema, Makuu, ya ajabu, matendo yako, ee Bwana Mungu Mwenyiezi; za haki, za kweli njia zako, ee Mfalme wa watakatifu.


Maana udizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa inchi na wa ulimwengu wofe, kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyiezi.


Nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, ee Bwana, ulioko, uliyekuwako, mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivu;


Nikaisikia madhbahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyiezi, za kweli, za haki hukumu zako.


Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, manti, na huzuni, na njaa, nae atateketezwa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni hodari.


Nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama farasi mweupe, nae aliyempanda, aitwae Mwaminifu na wa kweli, nae kwa haki ahukumu na kufanya vita.


Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Halleluya; kwa kuwa Bwana Mungu Mwenyiezi amemiliki.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo