Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 11:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Na katika saa ile palikuwa na tetemeko la inchi, nalo kubwa, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka, wana Adamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na khofu wakamtukuza Mungu wa mbingu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Wakati huohuo, kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu 7,000 wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Wakati huohuo, kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu 7,000 wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Wakati huohuo, kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu 7,000 wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Saa hiyo hiyo, kukawa na tetemeko kubwa la ardhi na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka. Watu elfu saba wakauawa katika tetemeko hilo, nao walionusurika wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Saa iyo hiyo, kukatokea tetemeko kubwa la nchi na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka. Watu elfu saba wakauawa katika tetemeko hilo, nao walionusurika wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 11:13
21 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi marra ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyu ni mwenye dhambi.


Siku zile akasimama Petro kati ya wanafunzi, akasema (jumla ya majina ilipata mia na ishirini),


Na baada ya siku tatu u nussu roho ya uhayi itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama, khofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.


Hekalu ya Mungu ikafunguliwa mbinguni na sanduku la agano likaonekana ndani ya hekalu yake. Kukawa umeme, na sauti, na radi, na tetemeko, na mvua ya mawe uyingi sana.


akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, kamtukuzeni, maana saa ya hukumu yake imekuja. Kamsujuduni yeye aliyezifanya mbingu na inchi na bahari na chemchemi za maji.


Ni nani asiyekucha, Bwana, na kulitukuza jina lako? kwa kuwa wewe peke yako Mtakatifu: kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele yako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.


Na tufurahi tukashangilie tukampe ulukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.


Lakini unayo majina machache, hatta katika Sardi, watu wasioyatia uchafu mavazi yao. Nao watakwenda pamoja nami katika mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.


Nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, tazama, palikuwa tetemeko kuu la inchi, jua likawa jeusi kama gunia la nywele, mwezi ukawa kama damu,


Malaika akakitwaa cheteso akakijaza moto wa madhbahu, akautupa juu ya inchi, kukawa sauti na radi na umeme na tetemeko la inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo