Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 1:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Tazama yuaja na mawingu: na killa jicho litamwona, na hawo waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amin.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Tazama! Anakuja na mawingu! Kila mtu atamwona, na hata wale waliomtoboa. Makabila yote duniani yataomboleza juu yake. Naam! Amina.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Tazama! Anakuja na mawingu! Kila mtu atamwona, na hata wale waliomtoboa. Makabila yote duniani yataomboleza juu yake. Naam! Amina.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Tazama! Anakuja na mawingu! Kila mtu atamwona, na hata wale waliomtoboa. Makabila yote duniani yataomboleza juu yake. Naam! Amina.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 “Tazama! Anakuja na mawingu,” na “kila jicho litamwona, hata wale waliomchoma”; na makabila yote duniani “yataomboleza kwa sababu yake.” Naam, ndivyo itakavyokuwa! Amen.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Tazama! Anakuja na mawingu, na kila jicho litamwona, hata wale waliomchoma; na makabila yote duniani yataomboleza kwa sababu yake. Naam, ndivyo itakavyokuwa! Amen.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 1:7
36 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.


ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni: ndipo mataifa yote ya ulimwengu wataomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbingu kwa nguvu pamoja na utukufu mwingi.


Hatta atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja nae, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake:


Yesu akamwambia. Wewe umesema: lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwoua Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu.


Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na nguvu nyingi na utukufu.


Yesu akasema, Mimi ndio yeye, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija na mawingu ya mbingu.


Ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu kwa nguvu na utukufu mwingi.


lakini askari mmoja kwa mkuki alimchoma ubavu, ikatoka marra damu na maji.


andiko la pili lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma.


na kumugojea Mwana wake kutoka mbinguni, ambae alimfufua katika wafu, Yesu, anaetuokoa na ghadhabu itakayokuja.


baada va haya sisi tulio hayi, tuliosalia, tutachukuliwa pamoja nao katika mawingu, illi tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.


Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa nayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho ya neema?


wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hatta wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu marra ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.


Wapenzi, sasa tu wana wti Mungu, wala haijadhihirika bado tutakidokuwa: lakini twajua ya kuwa akidhihiri, tutafanana nae; kwa maana tutamwona kama alivyo.


Na Enok, wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hawo, akisema, Angalia, Bwana alikuja na elfu kumi za watakatifu wake,


Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; Naja upesi. Amin: na uje Bwana Yesu.


Na watumishi wake watamtumikia; nao watamwona uso wake, na jina lake katika vipaji vya nyuso zao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo