Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 1:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, Baba yake: utukufu na ukuu una Yeye hatta milele na milele. Amin.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 akatufanya sisi kuwa ufalme wa makuhani, tumtumikie Mungu, Baba yake. Kwake Yesu Kristo uwe utukufu na nguvu, milele na milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 akatufanya sisi kuwa ufalme wa makuhani, tumtumikie Mungu, Baba yake. Kwake Yesu Kristo uwe utukufu na nguvu, milele na milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 akatufanya sisi kuwa ufalme wa makuhani, tumtumikie Mungu, Baba yake. Kwake Yesu Kristo uwe utukufu na nguvu, milele na milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 na akatufanya sisi kuwa ufalme na makuhani, ili tumtumikie Mungu wake ambaye ni Baba yake. Utukufu na uwezo ni vyake milele na milele! Amen.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 akatufanya sisi kuwa ufalme na makuhani, tumtumikie Mungu wake ambaye ni Baba yake. Utukufu na uwezo ni vyake milele na milele! Amen.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 1:6
23 Marejeleo ya Msalaba  

Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu.


illi wote wamheshimu Mwana kama wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyempeleka.


Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amin.


illi kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa liwima wetu Yesu Kristo.


killa ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.


ambae yeye peke yake hapatikani na mauti, akaae katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hapana mwana Adamu aliyemwona, wala awezae kumwona, ndiye mwenye heshima na uweza milele. Amin.


awafanye kuwa wrakamilifu katika killa tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, nae akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amin.


Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.


Uweza una yeye hatta milele na milele. Amin.


Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.


Yeye aliye Mungu pekee, mwenye hekima, Mwokozi wetu: kwake yeye utukufu, na ukuu, na uwezo, na nguvu kwa Yesu Kristo, tangu milele, na sasa, na hatta milele. Amin.


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Yu kheri, mtakatifu, aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watamiliki pamoja nae miaka elfu.


Umestahili, Bwana, Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na nweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, vikaumbwa.


ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa killa kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu: nao wanamiliki juu ya inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo