Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 1:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 aliyeshuhudia Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo, mambo yote aliyoyaona.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Naye Yohane ameshuhudia yote aliyoyaona kuhusu ujumbe wa Mungu na ushahidi wa Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Naye Yohane ameshuhudia yote aliyoyaona kuhusu ujumbe wa Mungu na ushahidi wa Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Naye Yohane ameshuhudia yote aliyoyaona kuhusu ujumbe wa Mungu na ushahidi wa Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 ambaye anashuhudia kuhusu kila kitu alichokiona, yaani neno la Mungu na ushuhuda wa Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 ambaye anashuhudia kuhusu kila kitu alichokiona, yaani, Neno la Mwenyezi Mungu na ushuhuda wa Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 1:2
22 Marejeleo ya Msalaba  

Yohana akashuhudu, akasema, Nimemwona Roho akishuka, kama hua, kutoka mbinguni; akakaa juu yake.


Bassi wakamshuhudia makutano waliokuwa pamoja nae alipomwita Lazaro kutoka kaburini akamfufua.


Nae aliyeona ameshuhudu, na ushuhuda wake ni kweli; na yeye anajua ya kuwa asema kweli, ninyi mpate kuamini.


Huyu ndiye mwanafunzi ayashuhudiae haya, na aliyeandika haya; na twajua ya kuwa ushuhuda wake ni wa kweli.


Amin, amin, nakuambia, Tulijualo twalisema, na tuliloliona twalishuhudu; na ushuhuda wetu hamwukubali.


Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia.


Lakini inuka, usimame, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke nwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo kwayo nitajidhihirisha kwako;


Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.


kama ushuhuda wa Kristo ulivyothubutika kwenu;


NAMI nilipokuja kwenu ndugu, sikuja niwakhubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.


ILIYOKUWA tangu mwanzo, tuliyoisikia, tuliyoiona kwa macho yetu, tuliyoitazama, na mikono yetu ikaipapasa, kwa khabari ya Neno la uzima,


Na sisi tumeona na kushuhudu ya kuwa Baba amempeleka Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu.


Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Na sisi pia twashuhudu, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli.


ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.


Bassi, yaandike mambo uliyoyaona, nayo yatakayokuwa baada ya hayo.


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; wala hawakupenda maisha yao hatta wakati wa kufa.


Joka akamkasirikia mwanamke akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo.


Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.


Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. Amin.


Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhbahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo