Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 1:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Mimi ni yeye aliye hai! Nilikuwa nimekufa, lakini, tazama, sasa ni hai milele na milele. Ninazo funguo za kifo na kuzimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Mimi ni yeye aliye hai! Nilikuwa nimekufa, lakini, tazama, sasa ni hai milele na milele. Ninazo funguo za kifo na kuzimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Mimi ni yeye aliye hai! Nilikuwa nimekufa, lakini, tazama, sasa ni hai milele na milele. Ninazo funguo za kifo na kuzimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Mimi ni Yeye Aliye Hai, niliyekuwa nimekufa, na tazama, ni hai milele na milele! Nami ninazo funguo za mauti na Kuzimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Mimi ni Yeye Aliye Hai, niliyekuwa nimekufa, na tazama, ni hai milele na milele! Nami ninazo funguo za mauti na kuzimu.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 1:18
32 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe Kapernaum, uliyeinuliwa hatta mbinguni, utashushwa hatta kuzimu: kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwako, ingalifanyika katika Sodom, ungalikuwapo hatta leo.


Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litafungwa mbinguni: na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.


Nao wakiingiwa na khofu na kuinama kifudifudi hatta inchi, wakawaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hayi katika wafu? Hayupo hapa, bali amefufuka.


Yesu akamwambia, Mimi ni ufufuo na uzima; aniaminiye mimi, ijapo afe, atakuwa ataishi,


Bado kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona; kwa sababu mimi ni hayi, ninyi nanyi mtakuwa hayi.


tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka hafi tena, mauti haimtawali tena.


Maana, ijapokuwa alisulibiwa katika udhaifu, illakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; bali tutaishi pamoja nae kwa uweza wa Mungu ulio ndani yenu.


Nimesulibiwa pamoja na Kristo, illakini ni hayi; wala si mimi tena, bali Kristo yu hayi ndani yangu; na uhayi nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.


Kwa maana mlikufa, na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.


Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


asiyekuwa kuhani kwa sharia ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na kikomo:


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


akaapa kwa yeye aliye bayi hatta milele na milele, aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na inchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na muhulla baada ya haya,


Na mmoja wa wale nyama wane wenye uliayi akawapa vichupa saba vya dhahabu, vimejaa ghadhabu ya Mungu aliye hayi hatta milele na milele.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Smurna andika; Haya ayanena yeye aliye wa kwanza na wa mwisbo, aliyekuwa amekufa, akawa hayi.


Bahari ikawatoa wafu waliomo ndani yake. Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu walio ndani yake. Wakahukumiwa killa mtu kwa kadiri ya matendo yao.


Mauti na Kuzimu wakatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Filadelfia andika; Haya ayanena yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daud, mwenye kufungua wala hapana afungae, nae afunga wala hapana afuuguae.


Na hawa nyama wenye uhayi watakapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi yeye aliye hayi hatta milele na milele ntukufu na heshima na shukrani,


Na wale nyama wane wenye uhayi wakasema, Amin. Na wale wazee ishirini na wane wakaanguka wakamsujudu yeye aliye hayi milele na milele.


Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Manti, na Kuzimu akafuatana nae. Wakapewa mamlaka juu ya robo ya inchi wane kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa nyama mwitu wa inchi.


MALAIKA wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya inchi; akapewa ufunguo wa shimo la abuso.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo