Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 1:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Na nilipomwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akiniambia, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Basi, nilipomwona tu, nilianguka mbele ya miguu yake kama maiti. Lakini yeye akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akasema, “Usiogope! Mimi ni wa kwanza na wa mwisho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Basi, nilipomwona tu, nilianguka mbele ya miguu yake kama maiti. Lakini yeye akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akasema, “Usiogope! Mimi ni wa kwanza na wa mwisho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Basi, nilipomwona tu, nilianguka mbele ya miguu yake kama maiti. Lakini yeye akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akasema, “Usiogope! Mimi ni wa kwanza na wa mwisho.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama aliyekufa. Ndipo akauweka mkono wake wa kuume juu yangu na kusema: “Usiogope, Mimi ndiye wa Kwanza na wa Mwisho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama aliyekufa. Ndipo akauweka mkono wake wa kuume juu yangu na kusema: “Usiogope, Mimi ndiye wa Kwanza na wa Mwisho.

Tazama sura Nakili

Ufunuo 1:17
30 Marejeleo ya Msalaba  

Marra Yesu akasema nao, akinena, Jipeni moyo; ni mimi; msiogope.

Na kwa kumwogopa walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu.

Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnanitafuta Yesu aliyesulibiwa.

Palikuwako mmoja wa wanafunzi wake, amemwegamia Yesu kifua chake, ambae Yesu alimpenda.

Na Petro akigeuka, akamwona mwanafunzi yule aliyependwa na Yesu akifuata; yeye ndiye aliyeegamia kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni na kusema, Bwana yu nani akusalitiye?

ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.

Yohana kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwake yeye alioko na aliyekuwako nii atakaekuwako: na zitokazo kwa roho saba zilizo mbele ya kiti chake cha enzi:

Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisiio, asema Bwana Mungu, alioko, aliyekuwako, na atakaekuwako, Mwenyiezi.

Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Smurna andika; Haya ayanena yeye aliye wa kwanza na wa mwisbo, aliyekuwa amekufa, akawa hayi.

Mimi Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo