Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 1:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Nae alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume: na upanga mkali, mkali kuwili, watoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua likingʼaa kwa nguvu zake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Katika mkono wake wa kulia alikuwa na nyota saba, na kinywani mwake mlitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake uling'aa kama jua kali kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Katika mkono wake wa kulia alikuwa na nyota saba, na kinywani mwake mlitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake uling'aa kama jua kali kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Katika mkono wake wa kulia alikuwa na nyota saba, na kinywani mwake mlitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake uling'aa kama jua kali kabisa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Katika mkono wake wa kuume alishika nyota saba, na kinywani mwake ulitoka upanga mkali wenye makali kuwili. Uso wake ulikuwa kama jua liking’aa kwa nguvu zake zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Katika mkono wake wa kuume alishika nyota saba, na kinywani mwake ulitoka upanga mkali wenye makali kuwili. Uso wake ulikuwa kama jua liking’aa kwa nguvu zake zote.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 1:16
26 Marejeleo ya Msalaba  

akageuka sura yake mbele yao: uso wake ukangʼaa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.


Ee Mfalme, wakati wa adhdhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote.


Tena ipokeeni chepeo ya wokofu, na upanga wa Roho, ndio neno la Mungu;


Maana Neno la Mungu li hayi, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko ukali wa upanga ukatao kuwili, tena lachoma kiasi cha kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.


Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhababu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, na vile vinara saba ulivyoviona ni makanisa saba.


NIKAONA malaika mwingine hodari akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake: na uso wake kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto.


NA ishara kuu ilionekana mbiuguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota thenashara.


Na upanga mkali hutoka kinywani mwake awapige mataifa kwa huo. Nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, nae anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ukali wa ghadhabu ya Mungu Mwenyiezi.


na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya farasi yule, utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.


KWA malaika wa kanisa lililo katika Efeso andika; Haya ayanena yeye azishikae nyota saba katika mkono wake wa kuume, aendae kati kati ya vile vinara saba vya dhahabu.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Pergamo, andika; Haya ayanena yeye aliye na upanga mkali, mkali kuwili;


Tubu; na usipotubu naja kwako upesi, nitafanya vita juu yako kwa upanga wa kinywa changu.


NA kwa malaika wa kanisa lililo katika Sardi, andika; Haya ayanena yeye aliye nazo roho saba za Mungu na zile nyota saba: Najua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hayi, nawe umekufa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo