Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 1:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 UFUNUO wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo kwamba hayana buddi kuwa upesi: akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumishi wake Yohana;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Huu ni ufunuo aliotoa Yesu Kristo, ambao Mungu alimpa awaoneshe watumishi wake mambo ambayo yanapaswa kutukia karibuni. Kristo alimtuma malaika wake amjulishe mtumishi wake Yohane mambo hayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Huu ni ufunuo aliotoa Yesu Kristo, ambao Mungu alimpa awaoneshe watumishi wake mambo ambayo yanapaswa kutukia karibuni. Kristo alimtuma malaika wake amjulishe mtumishi wake Yohane mambo hayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Huu ni ufunuo aliotoa Yesu Kristo, ambao Mungu alimpa awaoneshe watumishi wake mambo ambayo yanapaswa kutukia karibuni. Kristo alimtuma malaika wake amjulishe mtumishi wake Yohane mambo hayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Ufunuo wa Isa Al-Masihi aliopewa na Mungu ili awaoneshe watumishi wake mambo ambayo ni lazima yatukie hivi karibuni. Alijulisha mambo haya kwa kumtuma malaika wake kwa Yohana mtumishi wake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Ufunuo wa Isa Al-Masihi aliopewa na Mwenyezi Mungu ili awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo ni lazima yatukie hivi karibuni. Alijulisha mambo haya kwa kumtuma malaika wake kwa Yohana mtumishi wake,

Tazama sura Nakili




Ufunuo 1:1
30 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana mimi sikusema kwa nafsi yangu tu; bali yeye aliyenipeleka, yaani Baba, ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.


Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyosikia kwa Baba nimewaarifuni.


kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; wakavapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakaamini ya kwamba ndiwe uliyenituma.


Aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoshuhudia, wala hapana anaeukubali ushuhuda wake.


Nina maneno mengi ya kusema na kuhukumu katika khabari zenu; lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


Maana sikuipokea kwa mwana Adamu wala sikufundishwa na mtu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.


ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri ile, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache,


PAOLO, mtumwa wa Mungu, mtume wa Yesu Kristo, illi ienee imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli iletayo utawa,


Bassi, yaandike mambo uliyoyaona, nayo yatakayokuwa baada ya hayo.


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


AKAJA mmoja wa malaika wale saba wenye vile vichupa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi,


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Akaniambia, Andika, Wa kheri walioitwa kwa karamu ya arusi ya Mwana Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.


Nami Yohana nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemi mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.


Akaja mmoja wa wale malaika saba walio na vichupa vile saba vijaavyo yale mapigo saba ya mwisho, akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi arusi, mke wa Mwana kondoo.


AKANIONYESHA mto wa maji ya uzima, wenye kungʼaa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana kondoo.


Mimi Yesu nalimtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daud, ile nyota yenye kungʼaa ya assubuhi.


Akaniambia, Haya ni maneno ya uaminifu na ya kweli. Na Bwana Mungu wa manabii watakatifu alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumishi wake mambo ambayo hayana buddi kuwa upesi.


Na mimi Yohana ndimi niliye mwenye kuona haya na kuyasikia. Na niliposikia na kuyaona nalianguka nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha haya.


Akaniambia, Angalia, usifanye hivyo; mimi mjoli wako, na wa ndugu zako manabii na wa wale washikao maneno ya kitabu hiki. Msujuduni Mungu.


BAADA ya haya naliona, na tazama mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hatta huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana buddi kuwa baada ya bayo.


Akaja, akakitwaa kitabu katika mkono wa kuume wake aliyeketi juu ya kiti kile cha enzi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo