Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Tito 3:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda, bali kwa rehema yake, kwa josho la kuzaliwa kwa pili, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi, bali kwa sababu ya huruma yake, kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya kwa kutuosha kwa maji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi, bali kwa sababu ya huruma yake, kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya kwa kutuosha kwa maji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi, bali kwa sababu ya huruma yake, kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya kwa kutuosha kwa maji.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya rehema zake. Alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa mara ya pili na kwa kufanywa wapya kupitia kwa Roho Mtakatifu wa Mungu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya rehema zake. Alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa mara ya pili na kwa kufanywa wapya kwa njia ya Roho wa Mwenyezi Mungu,

Tazama sura Nakili




Tito 3:5
46 Marejeleo ya Msalaba  

Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


Na rehema zake vizazi hatta vizazi Kwao wanaomcha.


Kwa kukumbuka rehema Amemsaidia Israeli mtumishi wake,


Illi kuwatendea rehema baba zetu, Na kukumbuka agano lake takatifu;


Kwa rehema zake Mungu wetu, Kwazo mwangaza wa juu umetujia,


Huenda nikapata kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi vao.


Lakini ikiwa ni kwa neema yake, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema; na ikiwa ni kwa matendo, haiwi neema tena, au hapo matendo yasingekuwa matendo.


Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufunya upya nia zenu, mpate kujua kwa hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.


kwa maana hapana mwenye mwili atakaehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu, kwa matendo ya sheria: kwa maanii kujua dhambi kabisa huja kwa njia ya sharia.


Bassi, twahasibu ya kuwa mwana Adamu hupewa baki kwa imani pasipo matendo ya sharia.


Lakini kwa mtu asiofanya kazi, bali anamwammi yeye ampae haki asiye mtawa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.


kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, illi lisimame kusudi la Mungu la kuchagua,


Bassi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakae, wala wa yule apigae mbio, bali wa yule arehemuye, yaani Mungu.


Tuseme nini, bassi? Ya kwamba watu wa mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; yaani ile haki iliyo ya imani;


Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hizi; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa kuwa na haki katika jina la Bwana Yesu na katika Roho ya Mungu wetu.


tukijua ya kuwa mwana Adamu hafanyiziwi wema kwa matendo ya sharia, hali kwa imani ya Yesu Kristo, sisi tulimwamini Yesu Kristo illi tufauyiziwe wema kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sharia; maana kwa matendo ya sharia hapana mwenye mwili atakaefanyiziwa wema.


Lakini Mungu kwa kuwa mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda,


na mfanywe wapya kwa roho ya nia zenu,


kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno;


mkamvaa mtu mpya anaefanywa upya apate maarifa kwa mfano wake yeye aliyemumba.


aliyetuokoa akatuita kwa wito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake, tuliyopewa sisi katika Kristo Yesu, kabla ya nyakati za zamani;


Lakini wenia wa Mwokozi wetu Mungu na upendo wake kwa wana Adamu ulipoonekana,


tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa mwili kwa maji safi.


Bassi na tukikaribie kiti cha neema kwa nthubuitifu, illi tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.


wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hatta wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu marra ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.


Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambae kwa rehema zake nyingi alituzaa marra ya pili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuliwa kwake Yesu Kristo,


ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.


Mfano wa mambo haya ni ubatizo, nnaowaokoa na ninyi siku hizi; (sio kuwekea, mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo