Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Tito 2:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 wasiwe waibaji, bali wakionyesha uaminifu mwema wote, illi wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu katika mambo yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 au kuiba vitu vyao. Badala yake wanapaswa kuonesha kwamba wao ni wema na waaminifu daima, ili, kwa matendo yao yote, wayapatie sifa njema mafundisho juu ya Mungu, Mwokozi wetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 au kuiba vitu vyao. Badala yake wanapaswa kuonesha kwamba wao ni wema na waaminifu daima, ili, kwa matendo yao yote, wayapatie sifa njema mafundisho juu ya Mungu, Mwokozi wetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 au kuiba vitu vyao. Badala yake wanapaswa kuonesha kwamba wao ni wema na waaminifu daima, ili, kwa matendo yao yote, wayapatie sifa njema mafundisho juu ya Mungu, Mwokozi wetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 wala wasiwaibie, bali waoneshe kuwa wanaweza kuaminika kabisa, ili kwa kila namna wayafanye mafundisho ya Mungu Mwokozi wetu yawe ya kuvutia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 wala wasiwaibie, bali waonyeshe kuwa wanaweza kuaminika kabisa, ili kwa kila namna wayafanye mafundisho ya Mungu Mwokozi wetu yawe ya kuvutia.

Tazama sura Nakili




Tito 2:10
29 Marejeleo ya Msalaba  

Nani bassi aliye mtumishi yule amini mwenye haki, ambae bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape chakula kwa saa yake?


Vivi hivi nuru yenu iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wakamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.


Roho yangu yamfurahia Mungu, Mwokozi wangu.


Yule mtoto akakua akaongezeka nguvu rohoni; akawako majangwani hatta siku ya kutokea kwake kwa Israeli.


Aliye mwaminifu katika kile kilicho kidogo huwa mwaminifu na katika kile kilicho kikubwa: nae aliye mdhalimu katika kile kilicho kidogo, huwa mdhalimu na katika kile kilicho kikubwa.


Aliyasema haya, si kwa kuwahurumia maskini; hali kwa kuwa ni mwizi, nae ndiye aliyeshika mfuko, akavichikua vilivyotiwa humo.


Tena inayohitajiwa katika mawakili, ndio mtu aonekane amini.


BASSI nawasihini, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa,


Lakini mwenendo wenu uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, illi, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;


Khatimae, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya heshima, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye kuvuma vizuri, ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini haya.


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Bwana Yesu Kristo, tumaini letu;


Wazee watawalao vema wapewe heshima mardufu, khassa wao wajitaabishao kwa kukhutubu na kufundisha.


WO wote waiio chini ya mafungo, hali ya utumwa, wawahesabu bwana zao kuwa wamestahili heshima yote, jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu.


Mtu akifundisba mafundisho mengine, nae hayakubali maneno yenye afya va Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundislio yapatanayo na ntawa,


akalifunua neno lake kwa nyakati zake katika ule ujumbe nilioaminiwa mimi kwa amri ya Mwokozi wetu, Mungu:


Lakini wenia wa Mwokozi wetu Mungu na upendo wake kwa wana Adamu ulipoonekana,


mwe na maongezi mazuri kati ya Mataifa, illi, iwapo huwasingizia kuwa mnatenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa nae.


mkiwa na dhamiri njema, illi katika neno lile mnalosingiziwa kwamba m watenda mabaya, wataha yarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.


Killa aendeleae mbele, asidumu katika ma-fundisho ya Kristo, hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho ya Kristo, mtu huyu ana Baba na Mwana pia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo