Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Tito 1:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 kwa Tito, mwanangu katika imani tuishirikiyo: Neema na rehema na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo, Mwokozi wetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu wa kweli katika imani tunayoshiriki. Nakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu, Mkombozi wetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu wa kweli katika imani tunayoshiriki. Nakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu, Mkombozi wetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu wa kweli katika imani tunayoshiriki. Nakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu, Mkombozi wetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tunayoshiriki sote. Neema na amani zitokazo kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Mwokozi wetu, ziwe nawe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tunayoshiriki sote: Neema iwe kwako na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Al-Masihi Isa Mwokozi wetu.

Tazama sura Nakili




Tito 1:4
31 Marejeleo ya Msalaba  

maana leo katika mji wa Daud amezaiiwa Mwokozi kwa ajili yenu, ndiye Kristo Bwana.


Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako; maana tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika yake huyu ni Mwokozi wa ulimwengu.


yaani, tufarijiane mimi na ninyi, killa mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu.


kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu: Neema iwe kwenu na imani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwaua Yesu Kristo.


Nalimwonya Tito, nikamtuma yule ndugu pamoja nae. Je! Tito aliwatoza kitu? Hatukuenenda kwa Roho yeye yule na katika nyayo zile zile?


sikupata raha nafsini mwangu, kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali niliagana nao, nikaondoka kwenda Makedonia.


Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani, kama ilivyoandikwa. Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena;


Illakini Mungu, mwenje kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuwapo kwake Tito.


Lakini Mungu ashukuriwe atiae bidii ile ile kwa ajili yenu katika moyo wa Tito.


Bassi mtu akitaka khabari za Tito, yeye ni mshirika wangu, na mtenda kazi pamoja nami; tena akitaka khabari za ndugu zetu, wao ni mitume ya makanisa, na utukufu wa Kristo.


hatta tukamwonya Tito kuwatimilizieni neema hii kama vile alivyoianza.


Lakini Tito aliyekuwa pamoja nami, aliyekuwa Myunani, hakulazimishwa kutahiriwa:


Maana ninyi nyote ni wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo.


Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.


Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwaua Yesu Kristo.


kwa ndugu watakatifu na waaminifu, walio ndani ya Kolossai, Neema iwe kwenu na imani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.


Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu aliyenitia nguvu, kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akiniweka katika khuduma yake;


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kama alivyopenda Mungu, kwa ahadi ya uzima ulio katika Yesu Kristo:


kwa Timotheo mwanangu mpendwa; Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.


maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu wa sasa, akasafiri kwenda Thessaloniki; Kreske Galatia, Tito Daimatia.


akalifunua neno lake kwa nyakati zake katika ule ujumbe nilioaminiwa mimi kwa amri ya Mwokozi wetu, Mungu:


tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu, Mwokozi wetu Yesu Kristo;


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuuingia ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo.


Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua sana Bwana, Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.


Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.


mpate kuyakumbuka maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana Mwokozi iliyoletwa na mitume wake.


Na huu ndio njasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu kama vile apendavyo, atusikia:


Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia khabari ya wokofu wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikieni, illi niwaonye mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu marra moja tu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo