Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Tito 1:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Wanakiri kwamha wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana, ni wenye machukizo, maasi, na kwa killa tendo jema hawafai.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Watu kama hao hujidai kwamba wanamjua Mungu, lakini kwa matendo yao humkana. Ni watu wa kuchukiza mno na wakaidi, hawafai kwa jambo lolote jema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Watu kama hao hujidai kwamba wanamjua Mungu, lakini kwa matendo yao humkana. Ni watu wa kuchukiza mno na wakaidi, hawafai kwa jambo lolote jema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Watu kama hao hujidai kwamba wanamjua Mungu, lakini kwa matendo yao humkana. Ni watu wa kuchukiza mno na wakaidi, hawafai kwa jambo lolote jema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Wanadai kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Hao watu ni chukizo, wasiotii, wasiofaa kwa jambo lolote jema.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Wanadai kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Hao watu ni chukizo, wasiotii, wasiofaa kwa jambo lolote jema.

Tazama sura Nakili




Tito 1:16
27 Marejeleo ya Msalaba  

Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wuyafanye yasiyowapasa;


Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo maana; maana kwa sababu ya haya ghadhabu ya Mungu huwajia wana wa uasi.


nawe ufahamu neno hili, ya kuwa sharia haimkhusu mtu wa haki, bali maasi, mi wasio taratihu, na makafiri, na wenye dhambi, na wasio watakatifu, na wasiomcha Mungu, na wauao baba zao, na wauao mama zao, mi wauaji,


Lakini mtu asiyewatunza walio wake na khassa watu wa nyumba yake ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.


illi mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa illi atende killa tendo jema.


WAKUMBUSHE kujinyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa killa kazi njema,


Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, maasi, tumedanganywa, tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukienenda katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.


Yeye asemae, Nimemjua, nae hazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndani yake.


Kwa maana kuna watu wamejiingiza kwa siri, watu walioandikiwa zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufasiki, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.


Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyae machukizo na uwongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo