Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 9:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Nae Yesu, akijua mawazo yao, akasema, Jinsi gani mnawaza maovu mioyoni mwenu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Yesu aliyajua mawazo yao, akasema, “Kwa nini mnawaza mabaya mioyoni mwenu?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Yesu aliyajua mawazo yao, akasema, “Kwa nini mnawaza mabaya mioyoni mwenu?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Yesu aliyajua mawazo yao, akasema, “Kwa nini mnawaza mabaya mioyoni mwenu?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Lakini Isa akiyafahamu mawazo yao, akawaambia, “Kwa nini mnawaza maovu mioyoni mwenu?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Lakini Isa akiyafahamu mawazo yao, akawaambia, “Kwa nini mnawaza maovu mioyoni mwenu?

Tazama sura Nakili




Mathayo 9:4
24 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Killa ufalme ukifitinika na nafsi yake, hufanyika ukiwa; na killa mji au nyumba ikifitinika na nafsi yake, haitasimama.


Nae, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? nileteeni dinari niione. Wakaleta.


Marra Yesu akafahamu rohoni mwake kama wanafikiri hivi nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu?


Nae, akiyajua mawazo yao, akawaambia, Killa ufalme uliogawanyika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa, na nyumba iliyogawanyika nyumba kwa nyumba huanguka.


Yesu akafahamu fikara zao akajibu, akawaambia, Mnafikiri nini mioyoni mwenu?


Lakini yeye akatambua mawazo yao, akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Ondoka, kasimama katikati.


Yesu akajibu akamwambia, Simon, nina neno la kukuambia. Akanena, Mwalimu, sema.


Yesu alifahamu ya kwamba walitaka kumwuliza akawaambia, Hili ndilo mnalotafuta ninyi kwa ninyi, ya kuwa nalisema, Bado kitambo nanyi hamnioni, na bado kitambo na mtaniona?


Sasa tumejua ya kuwa unajua yote, wala huhitaji mtu akuulize; kwa hiyo twaamini ya kwamba ulitoka kwa Mungu.


Akamwambia marra ya tatu, Simon wa Yohana, Wanipenda mimi? Petro akahuzunika kwa kuwa alimwambia marra ya tatu, Wanipenda mimi? Akamwambia, Bwana, wewe unajua yote; unajua ya kuwa nakupenda. Yesu amwambia, Lisha kondoo zangu.


Yesu akajua nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanaliumigʼunikia neno hili, akawaambia, Neno hili linawachukiza?


Lakini kuna wengine miongoni mwemi wasioamini. Maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini na ni nani atakaenisaliti.


Petro akamwambia, Hikuwaje hatta mkapatana kumjaribu Roho ya Bwana? angalia, miguu yao waliomzika mume wako ipo mlangoni, nao watakuchukua wewe nawe.


nami nitawaua watoto wake kwa manti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzae viuno na mioyo. Nami nitampa killa mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo