Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 9:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Yesu alipokuwa anaondoka kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaaza sauti, wakinena. Uturehemu, Ee mwana wa Daud.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele, “Mwana wa Daudi, utuhurumie!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele, “Mwana wa Daudi, utuhurumie!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele, “Mwana wa Daudi, utuhurumie!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Isa alipokuwa akiondoka mahali pale, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti na kusema, “Mwana wa Daudi, tuhurumie!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Isa alipokuwa akiondoka mahali pale, vipofu wawili wakamfuata wakipiga kelele kwa nguvu na kusema, “Mwana wa Daudi, tuhurumie!”

Tazama sura Nakili




Mathayo 9:27
24 Marejeleo ya Msalaba  

KITABU eba ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daud, mwana wa Ibrahimu.


vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema.


Na mwanamke Mkauanaya wa mipaka ile akatokea, akampaazia sauti, akinena, Unirehemu. Bwana, Mwana wa Daud; binti yangu amepagawa sana na pepo.


Bwana, mrehemu mwana wangu, kwa kuwa hushikwa na kifafa, na kuteswa vibaya: maana marra nyingi huanguka motoni, na marra nyingi majini.


Hatta walipokuwa wakitoka Yeriko mkutano mkubwa wakamfuata.


Lakini makuhani wakuu na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto wakipaaza sauti zao hekaluni, wakinena, Utuokoe sasa, mwana wa Daud! wakakasirika,


Na makutano waliotangulia, na waliofuata, wakapaaza sauti zao, wakinena, Utuokoe sasa, Mwana wa Daud; amebarikiwa ajae kwa jina la Bwana; Utuokoe sasa wewe uliye juu.


Alipolika nyumbani, wale vipofu wakamwendea: Yesu akawaambia. Mnaamini kwamba naweza kufanya haya? Wakamwambia, Naam, Bwana.


umebarikiwa ufalme ujao kwa jina la Bwana, ufalme wa baba yetu Daud. Utuokoe sasa, wewe uliye juu.


Na marra nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno, utuhurumie, utusaidie.


nao wakapaaza sauti zao wakisema, Yesu, Bwana, uturehemu.


Akawaambia, Kwa maana gani hunena ya kwamba Kristo yu mwana wa Daud?


Saa ileile akawaponya watu wengi maradhi zao, na misiba yao, na pepo wabaya: na vipofu wengi akawakarimia kuona.


Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daud, na kutoka Bethlehemu, kijiji kile alichokaa Daud?


khabari za Mwana wake, aliyekuwa katika ukoo wa Daud kwa jinsi ya mwili,


na katika bao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili, aliye juu ya mambo yote, Mungu, anaehimidiwa milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo