Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 9:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Alipokuwa akiwaambia haya, yuaja jumbe mmoja, akamsujudia, akinena, Binti yangu udio kwanza afe: lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, uae atapona.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika, akamwinamia na kusema, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali twende umwekee mkono wako naye ataishi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika, akamwinamia na kusema, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali twende umwekee mkono wako naye ataishi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika, akamwinamia na kusema, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali twende umwekee mkono wako naye ataishi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Isa alipokuwa akiwaambia mambo haya, kiongozi wa sinagogi akaingia, akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini njoo uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Isa alipokuwa akiwaambia mambo haya, mara akaingia kiongozi wa sinagogi, akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini njoo uweke mkono wako juu yake, naye atakuwa hai.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 9:18
25 Marejeleo ya Msalaba  

Nao waliokuwa ndani ya chombo wakamwendea, wakamsujudia, wakinena, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.


Nae akaja akamsujudia, akinena. Bwana, nisaidie.


Nao walipoufikia mkutano, mtu akamjia, akampigia magoti, akinena,


Ndipo mama ya wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akimsujudia, akimwomba neno.


Nao walipomwona, wakamsujudia; lakini wengine waliona shaka.


Akaja mwenye ukoma akamsujudu, akinena, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.


Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakinena, Bwana, tuokoe tunaangamia.


Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; ikiwa watia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika: bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.


Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake.


akawaambia, Ondokeni: kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana.


Mkuu wa ile sunagogi akajibu, akiona hasira kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akawaambia makutano, Kuna siku sita itupasapo kufauya kazi: katika hizo, bassi, njoni mponywe wala si katika siku ya sabato.


Na mtu mkuhwa mmoja akamwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanyeni nipate kuurithi uzima wa milele?


Na mtumishi wa akida mmoja alikuwa hawezi, karibu kufa, nae ni mtu aliyependwa nae sana.


Yesu akamwambia, Mimi ni ufufuo na uzima; aniaminiye mimi, ijapo afe, atakuwa ataishi,


Bassi Mariamu, alipofika pale alipokuwapo Yesu, akamwona, akaanguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungaliwapo hapa, ndugu yangu asingalikufa.


Kiisha baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sunagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni.


Ikawa baba yake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paolo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, akamponya


Tufuate:

Matangazo


Matangazo