Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 8:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Maana na mimi ni mtu chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; au mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Maana, hata mimi niliye mtu chini ya mamlaka ya wengine, ninao askari chini yangu. Namwambia mmoja, ‘Nenda!’ Naye huenda; na mwingine, ‘Njoo!’ Naye huja; na mtumishi wangu, ‘Fanya kitu hiki!’ Naye hufanya.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Maana, hata mimi niliye mtu chini ya mamlaka ya wengine, ninao askari chini yangu. Namwambia mmoja, ‘Nenda!’ Naye huenda; na mwingine, ‘Njoo!’ Naye huja; na mtumishi wangu, ‘Fanya kitu hiki!’ Naye hufanya.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Maana, hata mimi niliye mtu chini ya mamlaka ya wengine, ninao askari chini yangu. Namwambia mmoja, ‘Nenda!’ naye huenda; na mwingine, ‘Njoo!’ naye huja; na mtumishi wangu, ‘Fanya kitu hiki!’ naye hufanya.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtu niliye chini ya mamlaka, nikiwa na askari chini yangu. Nikimwambia huyu, ‘Nenda,’ yeye huenda; na mwingine nikimwambia, ‘Njoo,’ yeye huja. Nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ yeye hufanya.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, nikiwa na askari chini yangu. Nikimwambia huyu, ‘Nenda,’ yeye huenda; na mwingine nikimwambia, ‘Njoo,’ yeye huja. Nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ yeye hufanya.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 8:9
17 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu aliposikia haya, akastaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa kama hii, hatta katika Israeli.


Akida akamjibu, akasema, Si stahili yangu wewe uingie chini ya dari yangu: lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.


Wakashangaa wote hatta wakaulizana, wakinena, Nini hii? Elimu hii mpya ni elimn gani? Maana kwa mamlaka awaamuru pepo wachafu nao wakamtii!


Akasimama karibu nae akaikemea ile homa, ikamwacha; marra akaondoka akawakhudumu.


Sababu mimi nami ni mtu aliyewekwa chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda: na huyu, Njoo, huja; na mtumishi wangu, Fanya hivi, hufanya.


AKAWAITA wale thenashara akawapa uweza na mamlaka juu ya pepo wote, na kuponya maradhi.


Ninyi watumwa, watiini wao ambao kwa niwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wana Adamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimeha Mungu.


Watumwa wawatii Bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo