Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 8:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Akida akamjibu, akasema, Si stahili yangu wewe uingie chini ya dari yangu: lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Huyo jemadari akamwambia, “Bwana, sistahili uingie nyumbani mwangu. Lakini sema tu neno, na mtumishi wangu atapona.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Huyo jemadari akamwambia, “Bwana, sistahili uingie nyumbani mwangu. Lakini sema tu neno, na mtumishi wangu atapona.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Huyo jemadari akamwambia, “Bwana, sistahili uingie nyumbani mwangu. Lakini sema tu neno, na mtumishi wangu atapona.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Lakini yule jemadari akamwambia, “Bwana, mimi sistahili wewe kuingia ndani ya nyumba yangu. Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu atapona.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Lakini yule jemadari akamwambia, “Bwana, mimi sistahili wewe kuingia chini ya dari yangu. Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu atapona.

Tazama sura Nakili




Mathayo 8:8
18 Marejeleo ya Msalaba  

Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


Lakini Yohana alikuwa akimzuia, akinena, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, na wewe waja kwangu?


Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa, akinena, Nataka: takasika. Marra ukoma wake ukatakasika.


Yesu akamwambia. Nitakuja, nimponye.


Maana na mimi ni mtu chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; au mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.


unifanye kuwa kama mmojawapo wa watumishi wako.


Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili baada ya hayo kuitwa mwana wako.


Simon Petro alipoona haya, akaanguka magotini pa Yesu, akasema, Toka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.


Ndiye ajae nyuma yangu, aliyekuwa mbele yangu, wala mimi sistahili niilegeze gidam ya kiatu chake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo