Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 8:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; illa enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, utoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Kisha Yesu akamwambia, “Angalia, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajioneshe kwa kuhani, na kutoa sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Kisha Yesu akamwambia, “Angalia, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajioneshe kwa kuhani, na kutoa sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Kisha Yesu akamwambia, “Angalia, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajioneshe kwa kuhani, na kutoa sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kisha Isa akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajioneshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Musa, ili kuwa ushuhuda kwao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kisha Isa akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Musa, ili kuwa ushuhuda kwao.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 8:4
31 Marejeleo ya Msalaba  

nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, illi kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.


Ndipo akawaagiza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ya kwamba yeye ndiye Yesu aliye Kristo.


Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaagiza, akinena, Msimwambie mtu khabari ya mambo hayo, hatta Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.


Yesu akajibu, akamwambia, Hayo yaache sasa: kwa kuwa hivi imetupasa kutimiza haki yote. Bassi akamwacha.


Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.


ANGALIENI msitoe sadaka zenu mbele ya watu, kusudi mtazamwe nao: kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.


Macho yao yakafumbuka. Yesu akawaagiza kwa nguvu, akinena, Angalieni hatta mtu mmoja asijue.


Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapelekeni maharazani: na katika masunagogi mtapigwa: na mtachukuliwa mbele za maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.


Akawagombeza sana, wasimdhihirishe.


Akawaagiza sana, mtu asijue khabari ile; akaamuru apewe chakula.


Na watu wote wasiokaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakungʼuteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu kuwa ushuhuda kwao.


Akawaagiza wasimwambie mtu; lakini kwa kadiri alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza khabari, wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena,


Akawaagiza wasimwambie mtu khabari zake.


Walipokuwa wakishuka mlimani akawaagiza wasimweleze mtu waliyoyaona, illa Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka katika wafu.


Alipowaona, akawaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa katika kwenda kwao wakatakasika.


Lakini haya yatapata kuwa ushuhuda wenu.


Pepo wakawatoka wengi wakipaaza sauti zao wakisema, Wewe u Kristo, Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walijua ya kuwa yeye ndiye Kristo.


Akamwagiza asimwambie mtu: illa enenda, ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe kwa kutakasika kwako alivyoamuru Musa, illi kuwa ushuhuda kwao.


Wazazi wake wakastaajabu sana, akawaamuru wasimwambie mtu lililotukia.


Petro akajibu, akasema, Kristo wa Mungu.


Sipokei utukufu kwa wana Adamu.


Yeye anenae kwa nafsi yake tu, hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anaetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyu ni wa kweli wala ndani yake hamna udhalimu.


Nami siutafuti ntukufu wangu; yuko atafutae na kuhukumu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo