Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 8:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Alipofika ngʼambu, katika inchi ya Wagergesene, watu wawili wenye pepo walikutana nae, wanatoka makaburini, wakali mno, hatta mtu asiweze kupita njia ile.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Yesu alifika katika nchi ya Wagadara, ngambo ya ziwa, na huko watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitokea makaburini. Watu hawa walikuwa wenye kutisha mno, hata hakuna mtu aliyethubutu kupita njia hiyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Yesu alifika katika nchi ya Wagadara, ngambo ya ziwa, na huko watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitokea makaburini. Watu hawa walikuwa wenye kutisha mno, hata hakuna mtu aliyethubutu kupita njia hiyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Yesu alifika katika nchi ya Wagadara, ng'ambo ya ziwa, na huko watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitokea makaburini. Watu hawa walikuwa wenye kutisha mno, hata hakuna mtu aliyethubutu kupita njia hiyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Walipofika ng’ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili waliopagawa na pepo wachafu walitoka makaburini nao wakakutana naye. Watu hawa walikuwa wakali mno kiasi kwamba hakuna mtu aliyeweza kupita njia ile.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Walipofika ng’ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili waliopagawa na pepo wachafu walitoka makaburini nao wakakutana naye. Watu hawa walikuwa wakali mno kiasi kwamba hakuna mtu aliyeweza kupita njia ile.

Tazama sura Nakili

Mathayo 8:28
9 Marejeleo ya Msalaba  

Khabari zake zikaenea katika Sham yote; wakamletea watu waliokuwa hawawezi, walioshikwa mi maradhi mbali mbali na mateso, nao wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.

Wale watu wakastaajabu, wakinena. Huyo ni mtu wa namna gani hatta pepo na bahari zamtii?

khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo