Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 8:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Akawaambia, Mbona mu waoga, enyi wa imani haba? Marra akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Yesu akawaambia, “Enyi watu wenye imani haba; mbona mnaogopa?” Basi, akainuka, akaukemea upepo na lile ziwa; kukawa shwari kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Yesu akawaambia, “Enyi watu wenye imani haba; mbona mnaogopa?” Basi, akainuka, akaukemea upepo na lile ziwa; kukawa shwari kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Yesu akawaambia, “Enyi watu wenye imani haba; mbona mnaogopa?” Basi, akainuka, akaukemea upepo na lile ziwa; kukawa shwari kabisa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Naye Isa akawaambia, “Kwa nini mnaogopa, enyi wa imani haba?” Kisha akaamka na kukemea dhoruba na mawimbi, nayo bahari ikatulia kabisa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Naye Isa akawaambia, “Kwa nini mnaogopa, enyi wa imani haba?” Kisha akaamka na kukemea dhoruba na mawimbi, nako kukawa shwari kabisa.

Tazama sura Nakili




Mathayo 8:26
24 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajua, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani haba, kwa sababu hamkuchukua mikate?


Yesu akawaambia, Kwa sababu ya kutokuamini kwenu. Kwa maana, amin, nawaambieni, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa hatta kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.


Lakini Mungu akiyavika hivi majani ya mashamba, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je, hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?


Wale watu wakastaajabu, wakinena. Huyo ni mtu wa namna gani hatta pepo na bahari zamtii?


Yesu akamkemea, akinena, Fumba kinywa, mtoke. Yule pepo akamwangusha katikati, akamtoka, asimdhuru.


Wala hakuionea shaka ahadi ya Mungu kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani yake, akimtukuza Mungu,


Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunuliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, na wa kushoto juu ya inchi,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo